Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Siri ya Aman Karume, Maalim Seif yafichuka, walipigwa mkwara kufikishwa The Hague

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
SIRI ya mapatano ya ghafla kati ya Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, yanayoelekea kuzaa serikali ya mseto visiwani, imefichuka.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na Tanzania Daima Jumatano, umebaini kuwa chanzo cha makubaliano ya ghafla ya viongozi hao imetokana na shinikizo kutoka nchi za Jumuiya ya Ulaya zilizotishia kuwafikisha katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), The Hague nchini, Uholanzi viongozi hao kama damu itamwagika tena katika uchaguzi mkuu ujao.
Tayari marais na viongozi kadhaa wa siasa barani Afrika, wamefikishwa katika mahakama hiyo kujibu tuhuma zinazowakabili za kusababisha umwagaji damu katika nchi zao.
Hadi kufikia Oktoba mwaka jana, nchi 110 zilisaini kukubali na kuitambua mahakama hii, ikiwemo Tanzania.
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa hadi sasa mahakama hiyo iliyoanza kutekeleza majukumu yake Julai Mosi 2002, The Hague nchini Uholanzi, imefungua uchunguzi katika maeneo manne ya Uganda Kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Afrika ya Kati na katika jimbo la Darfur.
Hadi sasa imewafikisha kizimbani watu wanaokadiriwa kufikia 10, saba wamebakia kama washtakiwa, wawili wanaaminika kuwa wamefariki dunia, wanne wako chini ya ulinzi na mmoja anatakiwa kuonekana kwa hiari mbele ya mahakama hiyo.
Kwa upande wa Afrika wapo viongozi wakuu kadhaa ambao mashtaka yao yamefikishwa mbele ya mahakama hii na kesi zao bado hazijaisha, akiwamo aliyewahi kuwa Rais wa Liberia, Charles Taylor; Makamu wa Rais wa zamani wa Kongo, Jean Pierre Bemba; na sasa anasakwa Rais wa Sudan, Omar al-Bashir
Mbali na hao wapo wapiganaji wa DRC waliofikishwa ICC ambao ni Thomas Lubanga, Germain Katanga na Mathieu Ngudjolo Chui.
Tags:

0 comments

Post a Comment