Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Papa ashutumu mswada wa Usawa Uingereza

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Papa Mtakatifu Benedicto wa Kumi na Sita ameishutumu serikali ya Uingereza kufuatia pendekezo la mswada mpya wa sheria, unaolenga kutoa usawa nchini humo.
Papa Benedict, amesema mswada huo utakuwa kikwazo kikubwa kwa makundi ya kidini kutekeleza majukumu yao kulingana na imani yao. Matamshi hayo yametolewa baada ya pendekezo la sheria mpya, itakayozuia ubaguzi wa kijinsia.
Kwa mfano kanisa Katoliki la Roma litazuiwa kuwabagua wapenzi wa jinsia moja na watu wanaobadilisha jinsia zao. Papa mtakatifu anasema sheria hiyo inakiuka desturi za kawaida za binadamu.
Lakini serikali ya Uingereza imesema mswada huo utaifanya Uingereza kuwa mahala pa haki na usawa kwa watu wote. Wakati huo huo kiongozi huyo wa kanisa Katoliki amethibitisha kuwa ataizuru Uingereza baadaye mwaka huu.
Ziara hiyo itakuwa ya kwanza kufanywa na Papa, tangu mwaka 1982 ambapo hayati papa John Paul wa pili aliitembelea nchi hiyo.
Tags:

0 comments

Post a Comment