Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Kibao chamgeukia Afande Kova Sakata la Muro!

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

Sakata la mwandishi wa habari za uchunguzi, Jerry Muro, limeingia katika hatua mpya baada ya wanasheria kusema kitendo chake cha kukutwa na pingu si kosa kwa mujibu wa sheria za nchi.

Muro, mfanyakazi wa Shirika la Utangazaji (TBC) na ambaye amejipatia umaarufu kutokana na kufichua aina tofauti za rushwa, Jumapili iliyopita alikutwa na pingu katika gari alilokuwa akilitumia mara baada ya kukamatwa kwa kudaiwa kutaka fedha kwa njia ya vitisho kwa aliyekuwa mhasibu wa Halmashauri ya Bagamoyo, Michael Wage.

Lakini wanasheria waliozungumzia sakata hilo wanapingana na maelezo hayo ya Kamanda Kova.

Wakizungumza jijini Dsm kwa nyakati tofauti, mawakili wa jijini Dar es salaam, Profesa Abdallah Safari na Mabere Marando walisema kwa mujibu wa sheria za nchini, hakuna kosa kwa mtu kukutwa na pingu.

"Kwa mujibu wa sheria za nchi, kukutwa na pingu si kosa ila utakuwa na kosa tena la jinai endapo ukikutwa na government stores (mavazi ya kijeshi na polisi ikiwemo kofia na mabuti) pamoja na kumiliki isivyo halali bunduki, bastola na hata risasi," alisema Profesa Safari.

Profesa Safari alifafanua kwamba katika mwenendo wa makosa ya jinai, hakuna kipengele kinachoonyesha kuwa ni kosa mtu kukutwa na pingu.

Naye Marando alisema hakuna kosa kukutwa na pingu kwa kuwa kifaa hicho ni kama bidhaa nyingine.

Alisema ndio maana duka la silaha huu vitu hivyo kwa hiyo kisheria si kosa kukutwa na pingu.

"Hakuna tatizo kukutwa na pingu kwa kuwa ni bidhaa na ndo maana inauzwa kwenye duka la silaha," alisema Marando.

Wakati hayo yakiendelea wanasheria wengine walisema Afande Kova amevunja Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007.

Kova amevunja sheria hiyo kwa kumtaja mtoa taarifa, Bw. Michael Wage, ambaye alidai kuombwa rushwa ya sh. milioni 10 na Bw. Muro.

Sheria hiyo kifungu cha 51 (1) (a) inazuia kutajwa kwa jina, makazi na anuani ya mtu aliyetoa taarifa kuhusu vitendo vya rushwa au aliyesaidia mamlaka inayohusika kufanikisha kukamatwa kwa mhusika.

Sehemu (b) ya kifungu hicho inazuia shahidi kujibu swali ambalo jibu lake linaweza kusababisha kujulikana kwa mtu aliyetoa taarifa juu ya vitendo vya rushwa.

Chanzo chetu kutoka ndani ya TAKUKURU kililimbia chano chetu kuwa kitendo kilichofanywa na Bw. Kova ni uvunjifu wa sheria hiyo.
Tags:

0 comments

Post a Comment