Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Mke wa Dk Slaa apata dhamana kugombea Ubunge kupitia CCM.

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
MKE wa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa, Rose Kamili, ambaye Diwani wa CCM wa Kata ya Bassotu, wilayani Hanang, amelituhumu jeshi la polisi wilayani Hanang kutumika kisiasa kutokana na kutekeleza maagizo ya kigogo mmoja kutaka yeye akamatwe pamoja na viongozi wa wafugaji.

Diwani huyo, ambaye ametangaza kugombea ubunge jimbo hilo la Hanang katika uchaguzi mkuu ujao kupitia CCM, alisema kukamatwa kwake juzi pamoja na wananchi wengine 13 ni shinikizo la kigogo huyo.

"Polisi wamenikata na kunipa dhamana mimi na Ally Kaoga jana na wamegoma kutoa dhamana kwa wananchi wengine 12 hili ni shinikizo la kigogo huyo tumepata taarifa amewaahidi baadhi ya wakulima kuwapa mashamba na wanataka kuzuwia dhamana ili walazimishe ugawaji wa mashamba," alisema Rose Kamili.

Kamili ambaye ni Diwani wa CCM tangu mwaka 1994 na amewahi kushika nyadhifa mbali mbali ndani ya CCM ikiwepo ujumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa, alisema mgogoro wa mashamba ya Hanang hivi sasa umefanywa wa kisiasa ili kuficha ukweli.

"Mimi nasema ugawaji wa mashamba Hanang uwe wa haki na wafugaji wapewe haki yao kwani kihistoria wao ndio walipokonywa na serikali maeneo yao na kuwafanya watawanyike karibu nchi nzima ili kuanzisha shirika la chakula la NAFCO," alisema Kamili.

Diwani huyo alisema kitendo cha kigogo huyo, kutembelea eneo la mgogoro kufanya mkutano wa hadhara juzi na kuahidi kuwashughulikia watu aliowaita wachochezi ni ishara kuwa suala hilo limekuwa la kisiasa.
Tags:

0 comments

Post a Comment