Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Misri bingwa tena Afrika yashinda 1-0 MFUNGAJI bora wa fainali za Afrika, Mohamed Nagui wa Ghana

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Emmanuel Agyemang-Badu (kushoto) wa Ghana akipiga mpira mbele ya Fathi wa Misri kwenye mchezo wa fainali za Mataifa ya Afrika CAN2010 zilizofanyika jana kwenye Uwanja wa November 11 mjini Luanda.

MFUNGAJI bora wa fainali za Afrika, Mohamed Nagui aliyeingia akitokea benchi na kufunga bao pekee kwa Misri liloipa ubingwa wa tatu mfululizo dhidi ya Ghana.

Chipukizi wa Ghana jana walithibisha ubora wao kwa kufanya kile kisochotegemewa na wengi baada ya kuwakabili vilivyo mabingwa wetetezi Misri kabla ya Mohamed Zidan kumtegenezea pasi nzuri Nagui aliyepiga shuti lilomshinda kipa Richard Kingson dakika ya 85.

Hilo lilikuwa bao la tatu kwa Nagui anafunga akitokea benchi na mawili alifunga kwenye mechi mbili alizoanza tangu mwanzo.

Misri iliyoingia kwenye mchezo huo ukipewa nafasi kubwa ya kushinda idadi kubwa ya mabao na kuchukuwa ubingwa huo kwa mara ya tatu mfululizo kirahisi.

Ghana waliingia kwenye mchezo wakitumia mbinu yao ya kulinda kwa umakini na kutibua mipango yote Misri walionekana kuzidiwa ujanja kwenye sehemu ya kiungo kufanya matokeo kuwa suluhu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili kilishudia ufundi mkubwa wa ndugu wawili Asamoah Gyan na mdogo wake Asamoah waliopoteza nafasi kadhaa za kufunga.

Dakika ya 73, beki wa kulia Samuel Inkoom alipitisha krosi nzuri lakini ilikosa umaliziaji.

Kiungo Eric Addo alikosa bao la wazi la kuisawazishia Ghana katika dakika ya 90 baada ya kupiga shuti mtoto kwa lilodakwa na kipa.

Kocha Hassan Shehata ametimiza ndoto yake ya kulitwaa taji hilo la Afrika kwa mara ya tatu kwa stahili ya aina yake huku timu yake ikiwa hajapoteza mchezo hata moja tangu mwaka 2008 walipochukuwa taji hilo nchi Ghana.

Misri pamoja na kutawala kwao soka ya Afrika watakuwa wakizishudia fainali za Kombe la Dunia zinazofanyika kwa mara ya kwanza kwenye ardhi ya bara hili kama watazamaji wengine.

Baada ya kukubalia kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Algeria kwenye mchezo uliochezwa nchini Sudan.

Nahodha wa Misri, Ahmed Hassan alichanguliwa kuwa mchezaji bora wa fainali hizo kwa mara ya pili mfululizo, huku Mohamed Nagui alipokea tuzo yake ya mfungaji bora wa fainali hizo za Angola kwa kufunga mabao matano.

Washindi wa tatu Nigeria walikabidhiwa medali za shaba juzi baada ya kuibwa Algeria kwa bao 1-0, Ghana walipokea medali za fedha kwa kushika nafasi ya pili.

Fainali zijazo za mataifa ya Afrika zitafanyika nchini Equtoria Guine kwa ushirikiano na Benin mwaka 2012.
Tags:

0 comments

Post a Comment