Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA MICHEZO - Yanga kutumia Sh146mil kwa miezi sita

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Yanga kutumia Sh146mil kwa miezi sita

Mwandishi Wetu

KLABU ya Yanga imepanga kutumia shilingi 145,974,500 kwa ajili ya kulipa mishahara ya wachezaji wake kuanzia mwezi Januari hadi Juni.

Katika mchanganuo uliotolewa hivi karibuni Yanga itatumia kiasi hicho cha fedha ikiwa ni mishahara ya wachezaji wake wa ndani na nje huku wachezaji wa benchi wakionekana kuchukua kiasi kikubwa cha fedha kuliko wale wanaocheza tena kwa kujituma.

Kati ya wachezaji hao, Kabongo Honore, Jama Mba wanaonekana kuchukua kitita kikubwa kuliko wakina Athuman Idd 'Chuji', Mrisho Ngasa na wengine ambao wamekuwa wakijituma zaidi uwanjani.

Wachezaji wa ndani pamoja na kujituma wamekuwa wakilipwa kiasi kinacholingana huku mchezaji Idd Mbaga na Ally Msigwa wakilipwa mshahara mdogo zaidi. Honore ndiyo mchezaji pekee anayelipwa fedha nyingi.

Mbali na mishahara, pia Yanga imepanga kukusanya kiasi cha shilingi 242,742,500 kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwa ni pamoja na mapato ya fedha za mechi za milangoni ikiwa za michuano ya Caf 'klabu bingwa Afrika', mechi za kirafiki, michuano ya Tusker, fedha za udhamini kutoka kampuni ya Bia Tanzania (TBL), pamoja na fedha za mauzo ya kadi za wanachama.

Pia klabu hiyo imepanga kutumia kiasi cha shilingi 965,823,000 kwa mwaka huu ikiwa ni kwa ajili ya usajili wa wachezaji wapya msimu mpya wa Ligi, nyongeza ya mishahara kwa wachezaji, benchi la ufundi, ikiwa ni pamoja na garama mbali mbali za uendeshaji.

0 comments

Post a Comment