Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Iran yatishia kutengeneza yenyewe nishati ya nyuklia

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

Iran yatishia kutengeneza yenyewe nishati ya nyuklia

TEHRAN

Iran imetoa muda wa mwisho kwa nchi za Magharibi kuukubali mpango wa kubadilishana uranium yake hafifu na nishati ya nyuklia kutoka nje, vinginevyo itatengeneza nishati yake ya nyuklia kwa ajili ya mtambo wa utafiti mjini Tehran.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Ujerumani amesema muda huo uliotolewa na Iran hautabadilisha msimamo wa mataifa ya Magharibi. Amesema, pendekezo la jumuiya ya kimataifa kwa Iran kuwa madini yake ya Uranium ambayo hayakurutubishwa kamili, yasafirishwe Urusi na Ufaransa ili yapate kurutubishwa zaidi kwa matumizi yake ya nishati, bado liko pale pale.

Marekani na nchi kadhaa za Magharibi zinaituhumu Iran kuwa inataka kutengeza silaha za nyuklia kwa kisingizio cha kuzalisha nishati ya umeme. Jamhuri hiyo ya Kiislamu ya Iran, inakanusha kabisa madai hayo na inasisitiza kuwa mpango wake wa nyuklia ni kwa ajili ya uzalishaji wa umeme.

Tags:

0 comments

Post a Comment