Silaa-Mimi na CCM, wao na mimi
Alisema kuwa ataendelea kufichua ufisadi unaofanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwan ameendelea kuwaweka tumbo joto viongozi wa CCM, baada ya kutangaza kuwa ameanza kuchunguza mali zote za chama hicho kama zililipiwa kodi na kisha ataweka mambo hadharani. Si mwingine bali ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, pia ni Mbunge wa Kratu (Chadema) Vile vile, amesema (CCM), inapaswa kulipa kodi ya Sh. bilioni sita kwa magari 200 iliyoagiza badala ya bilioni 1.7 kama ilivyotangazwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba. Dk. Slaa alisema atafuatilia hadi dakika ya mwisho kuhakikisha CCM kinalipa kodi hiyo ili iweze kuwanufaisha Watanzania wengi maskini. “Sitaki malumbano na mtu yeyote, ninachotaka kuona ni CCM inalipa kodi yote hiyo ili shule, hospitali, barabara na huduma zingine za jamii zipatikane,” alisema Dk. Slaa. Alisema Operesheni Sangara iliyoendeshwa katika wilaya zote za mkoa huo pamoja na Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Dk. Slaa alikaririwa na vyombo mbalimbali vya habari akisema kuwa CCM kimeingiza nchini magari 200 kwa ajili ya kampeni za uchaguzi mkuu wa mwakani bila kulipia ushuru wa Sh. milioni 600. Alisema kama Makamba alisema walilipa kodi ya bilioni 1.7 alipaswa kuwaeleza waandishi wa habari kiasi cha jumla ya kodi yote ya magari 200 waliyopaswa kuilipa. Kuhusu kauli ya CCM iliyotolewa na kuwa haitamshitaki kwa kuwa aibu iliyompata mbele ya jamii kwa kusema uongo inatosha, Dk. Slaa alisema hawezi kulumbana na Katibu wa Idara ya Uchumi na Fedha ya Halmashauri kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Amos Makala, kwa kuwa sio saizi yake. Alisema kwa sasa yeye si kujibishana na mtu kama huyo maana si saizi yangu kwani wananchi ndio wataamua nani kapata aibu kati yangu na CCM na kwa taarifa yao nitaendelea kuchunguza ukwepaji wao kodi.
0 comments