IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
MAJOZI huzuni vilitalawa kila kona ya jijini Luanda wakati wenyeji wa fainali za Afrika 2010, Angola walipokubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Ghana na kuaga michuano hiyo.
Nyota wa Black Stars, Asamoah Gyan alifunga bao hilo pekee dakika ya 16, akipokea pasi ndefu kutoka kwa mdogo wake Kwadwo Asamoah.
Katika mchezo huo Angola walijitahidi kufanya mashambulizi mengi kupitia kwa washambuliaji wake Manucho na Flavio lakini walipoteza umakini kwenye umaliziaji.
Dakika ya 44, Flavio akiwa ndani ya eneo la hatari alimtegeneza pasi nzuri Manucho aliyepiga shuti lilopaa juu ya goli.
Katika mchezo huo Manucho alipoteza nafasi nyingi za kufunga alilozipata akiwa yeye na kipa.
Nahodha wa Angola, Kali nusu aisawazishia nchi pale alipomzidi ujanja kipa Richard Kingston, lakini beki Isaac Vorsah alifanya kazi ya ziada kutoa nje mpira huo.
Wakati huo huo; Leo kutakuwa na mechi mbili zenye kukumbusha fainali zilizopita za mataifa ya Afrika, mchezo wa Zambia dhidi ya Nigeria unakumbusha fainali ya mwaka 1994 wakati huo kocha wa Simba, Partick Phiri akiwa kipa wa Chipolopolo.
Leo watashuka dimbani bila ya kiungo wao tegemeo Rainfrod Kabala mwenye kadi nyingi za njano.
Huku Cameroon wanaingia uwanjani wakiwa ni kumbukumbu ya kufungwa mabao 4-2 kwenye hatua ya Makundi na 1-o siku ya fainali na Misri mwaka 2008 nchini Ghana.
Tayari mshambuliaji Samwel Eto'o amewataka wachezaji wenzake kusahau yaliyopita na wajipange upya kwa mchezo huo muhimu.
You Are Here: Home - - Wenyeji Angola wabamizwa Fainali za kombe la Afrika hatua ya nusu fainali.Ghana 1-0 Angola
0 comments