Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Risasi yafyetuka na kuua askari magereza wawili

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Risasi yafyetuka na kuua askari magereza wawili
Mwandishi Wetu, Sumbawanga, Rukwaa

ASKARI magereza wa gereza la mahabusu wilayani Mpanda, Elias Mwananjela anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 48 na Sotas Stao (26), wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya risasi kufyetuka na wakati wakisafiri kwa mwendo kasi na gari kupitia barabara ya Tawakali wilayani Mpanda.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka katika eneo hilo, na kuthibitishwa kwa njia ya simu na Kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa Isunto Mantage, tukio hilo, lilitokea January 4, saa 7:00 mchana wakati marehemu huyo na wenzake watatu wakiwa wanatoka kuchukua fedha katika benki ya NMB tawi la Mpanda.

Walilitaja gari hilo, lililopinduka kuwa ni namba STK 4401 Had top mali ya gereza hilo, wilayani Mpanda na kuwa lilikuwa likiendeshwa na Sotas Stao .

Waliojeruhiwa katika tukio hilo baada ya risasi kufyatuka na gari kupinduka ni Said Jumanne (34) ambaye alikuwa amebeba bunduki hiyo, iliyosababisha kifo, na mhasibu wa gereza hilo, Pande Gundula (47).

Taarifa zilizopatikana kutoka katika eneo hilo, zilibainisha kuwa chanzo cha tukio hilo ni mwendo kasi wa gari hilo, pamoja na uzembe wa dereva huyo.

Muuguzi Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Pius Buzimale alikiri kupokea majeruhi watatu pamoja na maiti moja na kuongeza kuwa hali za majeruhi wawili si nzuri na kuwa wamelezwa katika wodi ya wagonjwa mahuthuti ya hospitali hiyo.

Naye Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa Isunto Mantage alisema fedha zilizochukuliwa benki kwa ajili ya matumizi ya gereza hilo, zimeokolewa na kuongeza kuwa uchunguzi zaidi wa tukio hilo, unaendelea na kuwa taarifa zaidi za tukio hilo, zitatolewa baada ya uchunguzi wa jeshi hilo, kukamilika.

Tags:

0 comments

Post a Comment