Iran yafuta ziara ya ujumbe wa Ulaya
WASHINGTON
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton, amesema kuwa nchi hiyo imeanza kujadiliana na washirika wake wa kidiplomasia juu ya kuiwekea Iran vikwazo vipya.
Bibi Clinton amesema kuwa nia ni kuiwekea mbinyo serikali ya Iran bila ya kuathiri maisha ya wananchi wa kawaiada wa Iran.
Wakati huo huo, ziara ya ujumbe wa bunge la Umoja wa Ulaya kutembelea Iran, bila ya kutegemewa imezuiwa na serikali ya nchi hiyo.
Shirika la habari la Irana limesema kuwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imeaihirisha kuwepo kwa ziara hiyo, ili kutoa nafasi kwa maandalizi zaidi ya kuukaribisha ujumbe huo.
Hata hivyo, kiongozi wa ujumbe huo wa bunge la Umoja wa Ulaya, Barbara Lochbihler, amesema kuwa ziara hiyo imesitishwa baada ya Iran kuzuia kuwepo mkutano kati ya ujumbe wake na baadhi ya viongozi wa upinzani nchini Iran.
0 comments