Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Rais wa Benki ya Dunia kuzuru Manzese

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

WAKATI Rais wa Benki ya Dunia, Robert Zoellick anatarajia kuzuru Manzese jijini Dar es Salaam wiki ijayo, wajumbe wa mitaa ya Mwembeni na Midizini wamegoma kushiriki shindano la usafi kwa mitaa minane ya kata hiyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwa sharti la kutotaja majina yao gazetini, wajumbe hao walisema hatua ya kufanya usafi ni ya zimamoto kwa sababu tukio hilo linatakiwa kufanyika mara kwa mara.
Walisema pamoja na kutolewa kwa shindano hilo, lakini mitaa hiyo haikidhi haja ya kuwa mitaa licha ya kuwekwa kwenye ratiba ya kutembelewa na Zoellick.
Mshindi wa kwanza wa shindano hilo anatarajiwa kuzawadiwa sh 150,000 wakati mshindi wa pili atajinyakulia vifaa vyenye thamani ya sh 100,000.
Mitaa iliyotajwa kushiriki shindano hilo ni Uzuri Chakula bora, Mnazi Mmoja, Mvuleni, Kilimani, Muungano, Manzese Uzuri, Midizini na Mwembeni. Hata hivyo mitaa ya Mwembeni na Midizini imegoma kushiriki.
Walisema kabla ya ujio huo, wameshauri Ofisi ya Waziri Mkuu itembelee mitaa ya Manzese na ijionee hali ilivyo kwa sasa.
Mradi huo umefadhiliwa na Benki ya Dunia ambayo ilitoa sh milioni 600, Halmashauri ya Kinondoni ilitoa sh milioni 334 na wananchi walitakiwa kuchangia sh milioni 334
Tags:

0 comments

Post a Comment