Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Malawi yaicharanga Algeria 3-0

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Malawi yaicharanga Algeria 3-0
Malawi waliopewa nafasi finyu wamewapa ugonjwa wa moyo Algeria moja ya timu zinazopewa nafasi ya kufanya vizuri katika mashindano ya soka ya Mataifa ya Afrika.

Malawi wamefanikiwa kuwalaza Algeria kwa mabao 3-0 katika mchezo uliohudhuriwa na watazamaji wacheche mjini Luanda.

Russel Mwafulirwa alifanikiwa kutumia makosa ya walinzi wa Algeria katika dakika ya 17 na kupachika kupata bao la kwanza kwa shuti kali.

Alikuwa ni Elvis Kafoteka aliyemalizia kwa kichwa bao la pili na kuwaweka Malawi katika nafasi ya kujiamini.

David Banda alitumia tena makosa ya walinzi wa Algeria katika kipindi cha pili na kupachika bao la tatu kwa mpira uliokuwa ukiviringika na kumshinda mlinda mlango wa Algeria Faouzi Chaouchi.

Viti vingi vilikuwa havina watu uwanjani hali iliyoonesha Waangola hawakwenda uwanjani kutokana na kupigwa mshangao kwa matokeo ya Jumapili walipolazimishwa sare na Mali ya mabao 4-4 katika mchezo wa ufunguzi.
Tags:

0 comments

Post a Comment