IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) juzi kiliuteka mji mdogo wa Bomang’ombe wilayani hapa baada ya kufanya maandamano makubwa yaliyojumuisha baiskeli, pikipiki na bajaji zaidi ya 100.
Maandamano hayo yaliyokuwa na lengo la kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura yaliongozwa na Mwenyekiti chama hicho, Freeman Mbowe ambaye pia alitangaza kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu ujao.
Yalianzia ofisi za wilaya za chama hicho na kupita mitaa mbalimbali na kumalizikia viwanja vya Sokoni kulipofanyika mkutano mkubwa wa hadhara.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Mbowe alisema si sahihi kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kujivunia umaskini wakati alikuwa mtumishi wa Ikulu miaka 25, mbunge na waziri kwa miaka 10.
‘Ni aibu Pinda kujivunia umaskini wakati alikuwa waziri kwa miaka kumi, amekuwa mtumishi Ikulu miaka 25 anatuambia leo kwa kipindi chote hicho hakujenga nyumba, aliishi chumba kimoja alichopewa na babu yake huyu,” alisema Mbowe.
Alisema kuna mifumo mibaya ya kupata viongozi ambayo mara nyingi huishia kuwaumiza wananchi akitolea mfano Rais Jakaya Kikwete kumteua Mbunge wa Iringa Mjini, Monica Mbega kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, jambo ambalo alisema si sahihi kutokana na mbunge huyo kutumia muda mwingi kuwatumikia wapiga kura wake.
You Are Here: Home - - CHADEMA yazidi kutesa K'njaro
0 comments