Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Yanga na Simba...

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Usajili wa CAF: Simba wachezaji 27, Yanga 29
Mwanachama wa friends of Simba, Geofrey Nyange (Kaburu) akiwa na Mike Baraza walipotua katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana Jumatatu, alikwenda Nairobi kumfuata Baraza ambaye amesaini kucheza Simba.
Na Mwandishi Wetu SIMBA na Yanga zimefanya usajili kwa kuongeza wachezaji wawili tu kila upande, lakini usajili wa dirisha dogo ulifungwa rasmi jana Jumatatu. Simba imewasajili Mike Baraza na Jerry Santo wote kutoka Kenya huku Yanga ikiwasajili John Njoroge na kipa wa Ghana, Ywa Derko. Huu ndio usajili wote wa klabu hizo mbili ambao mwezi huu utatumiwa pia katika Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ambapo Yanga itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na Simba itashiriki Kombe la Shirikisho. Mchezaji anayecheza katika mashindano yoyote ya CAF, lazima awe pia amesajiliwa na klabu yake kwa mashindano ya ndani. Huu ndio usajili kamili wa Yanga na Simba SIMBA 1.Juma Kaseja 2.Haruna Shamte 3.Haruna Moshi 4.Salum Kanoni 5.Kelvin Yondan 6.Salim Aziz 'Gilla' 7.Danny Mrwanda 8.Nico Nyagawa 9.Uhuru Seleman 10. Mussa Mgosi 11.Hilary Echesa 12.Ulimboka Mwakingwe 13.Antony Matangalu 14.Mohamed Banka 15.Ramadhan Chombo 16.Ally Mustapha 17.Joseph Owino 18.Jabir Aziz 19.Deogratius Mushi 20.Juma Jabu 21.Juma Nyosso 22.Emmanuel Okwi 23. Mohamed Kijuso 24.David Naftali 25. Amir Kiemba 26.Mike Baraza (mpya) 27.Jerry Santo (mpya) WALIOACHWA 1.Meshack Abel- Amekwenda African Lyon kwa mkopo 2.George Nyanda-Amekwenda African Lyon kwa mkopo 3.Adam Kingwande-Amekwenda African Lyon kwa mkopo YANGA 1. Ally Msigwa 2. Steven Marashi 3. Bakari Mohamed 4. Nadir Haroub 5. Wisdom Ndhlovu 6. Athuman Idd 7. Nurdin Bakari 8.Kabongo Honore 9. Steven Bengo 10. Robert Jama Mba 11.Boniface Ambani 12. Fred Mbuna 13.Geofrey Bonny 14. Mrisho Ngassa 15. Moses Odhiambo 16. Amir Maftah 17. Obren Cuckovic 18. John Njoroge (Mpya) 19. Shadrack Nsajigwa 20. Iddy Ally 21. Abdi Kassim 22. Nelson Kimath 23. Kigi Makasi 24. Shamte Ally 25. Hamisi Yusuph 26. Razak Khalfan 27. Jerry Tegete. 28.George Owino 29.Ywa Derko (Mpya) WALIOACHWA 1. Mike Baraza-Mkataba umekwisha 2.Vicent Barnabas-Kwa mkopo African Lyon 3.Joseph Shikokoti- Ameondoka
Tags:

0 comments

Post a Comment