Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Waasi Wamuua Gavana nchini Colombia

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Maafisa wa Colombia wamepata maiti ya gavana wa jimbo la kusini la Caqueta, Luis Francisco Cuellar.

Kiongozi huyo alitekwa nyara kutoka makaazi yake hapo jumatatu na watu walioshukiwa kuwa waasi wa mrengo wa kushto wa FARC.

Maiti ya gavana huyo ilipatikana ikiwa imekatwa koo na kufungwa mabomu. Rais wa Colombia Alvaro Uribe amesema kitendo hicho hakitahujumu harakati za serikali dhidi ya waasi wa FARC.

Maiti ya gavana huyo ilipatikana kilomita 15 kutoka makaazi yake na watekaji nyara wake wametoweka licha ya msako mkali wa polisi.

Bw. Cuellar ndiye gavana wa kwanza kuawa na waasi hao tangu rais Uribe kutwaa madaraka ambapo aliahidi kuimarisha demokrasia nchini Colombia.

Tags:

0 comments

Post a Comment