Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - silaha kali za kivita zaidi ya 35 zakutwa shambani mkoani Lindi. zilitumika wakati wa vita ya kwanza ya dunia (mwaka 1914 hadi 1918)

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Inatisha sana!!! au ndo funga mwaka?

Linaonekana lenyewe ni miongoni mwa matukio ya aina yake katika kuelekea mwishoni mwa mwaka 2009, kwa kitendo cha silaha 35 za kivita kukutwa ndani ya shamba la mtu mmoja mkoani humo. Silaha hizo zilikamatwa na polisi wa mkoa huo wa Lindi zikiwemo 35, ni pamoja na bunduki za Kijerumani aina ya Mark 4 yakiwemo na mabaki ya risasi kadhaa. Kamanda wa Polisi mkoani Lindi, Sifuel Shirima, amesema silaha hizo zimepatikana hivi karibuni, mishale ya saa 4:00 asubuhi, katika shamba hilo lililopo kwenye Kijiji cha Mahiwa, Kata ya Nyangao, wilaya ya Lindi. Alisema kuwa mkulima mmoja wa kijiji hicho aitwaye Elias Sita, 29, alikuwa akiendelea na shughuli zake za shamba kama kawaida na ndipo alipobaini kugonga kwa jembe kitu kigumu ardhini. Mkulima huyo alibaini kuwa alichokigonga ni bunduki, hivyo akaogopa na mara moja akachukua hatua ya kwenda kutoa taarifa katika ofisi ya Serikali ya Kijiji, kisha taarifa hizo zikatua polisi. Katika kile kinachoonekana kuwa lenyewe ni miongoni mwa matukio ya aina yake katika kuelekea mwishoni mwa mwaka 2009, polisi mkoani Lindi wamenasa silaha 35 za kivita toka kwenye shamba la mtu mmoja mkoani humo. Akasema kuwa baadaye, mkulima huyo alibaini kuwa alichokigonga ni bunduki, hivyo akaogopa na mara moja akachukua hatua ya kwenda kutoa taarifa katika ofisi ya Serikali ya Kijiji, kisha taarifa hizo zikatua polisi. Kamanda huyo akasema baada ya hapo, polisi kutoka wilayani walienda katika eneo hilo la tukio na kuchimba ardhini, ambapo waligundua bunduki 35 aina ya Mark 4 na risasi zaidi ya tano. Bunduki hizo ambazo ni za kijerumani, zilikuwa zimebakia mitutu baada ya sehemu ya mbao zake kuanza kuliwa na wadudu. Na wao wanaamini kuwa chanzo cha kuwepo kwa silaha hizo za kivita, ni kwamba eneo hilo lilitumika kwa mapigano wakati wa vita ya kwanza ya dunia (mwaka 1914 hadi 1918). Wakati huo huo, wataalam kadhaa wa silaha toka Jeshi la Wananchi (JWTZ) na wale wa Jeshi la Polisi wanatarajiwa kufika katika eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Kamanda Shirima amesema lengo la kutumwa kwa wataalama hao, ni kujihakikishia kuwa eneo hilo ni salama na halina mabaki zaidi ya silaha kama hizo za kivita na nyinginezo zinazoweza kuhatarisha maisha ya raia na mali zao.

Tags:

1 comments

  1. Anonymous says:

    acheni utoto,nyie mnafikiri sherehe ni kula tuu????????mna mambo gani mengine ya kuwa kivutio

Post a Comment