Habari nyingine iliyoifikia THE THOMCOM Inc. inasema kwamba chuo kikuu cha urafiki Lumumba (Moscow Russia) kimeapa kuwatimua chuo wanafunzi 76 watanzania watfukuzwa shule ifikapo tarehe 15/12/2009 kama wanafunzi hao watakuwa hawajalipa ada ya mwaka uliopita. Uongozi wa chuo umesema enzi za kuwadekeza watanzia zimekwisha na sasa wanafunzi wote wataadhibiwa kwa usawa. Akiongea na THE THOMCOM Inc. Mkuu wa kitengo cha ushirikiano wa kimataifa amesema chuo kinawadai watanzania hao dola za kimarekani 120 387.69 Notisi ya kuwafukuza chuo wanafunzi hao kwa kula ada imetolewa na Denisenko V.N. ambaye ni msaidizi wa mkuu wa chuo kwa maswala ya ushiriano wa kimataifa na kusainiwa na mkuu wa chuo Akademiki Filippov V.M.
Imeandaliwa na kutolewa na mwandishi wetu
0 comments