Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Mdogo wa Kingunge aionya CCM

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

MDOGO wa mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale – Mwiru; Enock Ngombale, ametoa onyo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwa huenda kikafanya vibaya kwenye uchaguzi mkuu ujao kutokana na hali ya kisiasa inayoendelea ndani ya chama hicho.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano, Dar es Salaam jana, alisema hali ya wasiwasi kwa CCM kufanya vibaya inatokana na hatua ya kushindwa kuelewana kwa baadhi ya wagombea wa nafasi mbalimbali kwenye chaguzi za serikali za mitaa.

“Kama hali ya mambo ndani ya chama itazidi kuwa mbaya kwa hatua hii ya kuwania nafasi kwenye serikali za Mitaa, hivyo nina wasiwasi kwa chama kumeguka na kusambaratika,” alisema Ngombale ambaye pia ni kada wa chama hicho.

Ngombale alibainisha kwamba, kutokana na hali ya wazee na vijana kubadilika kifikra, wanasiasa wengi watakuwa kwenye wakati mgumu wa kuchaguliwa.

“Kama utagundua, sasa hivi kumekuwapo na migongano ya kauli kati ya viongozi wa ngazi ya juu, wakiwamo wabunge, kuhusu kupinga suala la ufisadi.

“Mimi ni kada wa CCM, lakini hali hii ya mambo ndani ya chama, nawataadharisha viongozi wa juu kuchukua hatua ya haraka kukinusu chama kabla ya kusambaratika…tusipoziba ufa, tutajenga ukuta,” alisema kada huyo aliyewahi kuwa mtangazaji maarufu wa redio ya taifa.

Tags:

0 comments

Post a Comment