Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Dk Slaa atangaza hana mpango wa kugombea urais 2010

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Dk Slaa atangaza hana mpango wa kugombea urais 2010
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willbrod Slaa, hafikiri kugombea urais.
Na Patricia Kimelemeta

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willbrod Slaa, amevunja ukimya na kueleza kuwa hafikirii kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwakani.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Dk Slaa ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Karatu, alisema "Ikulu si mahali pazuri kukimbilia na urais si mchezo wa kitoto."

Alisema wakati alipojiundoa katika upadre na kujitumbukiza katika ulimwengu wa kawaida, aliahidi kuwatumikia wananchi wa Karatu na si kutafuta njia ya kuingia Ikulu, ambako alisema kuna matatizo mengi yanayoweza kumfanya mtu kukosa usingizi.

“Unajua Ikulu si lele mama, kunahitaji mtu mvumilivu hasa wananchi wake wanapohangaika na ugumu wa maisha ya kila siku, jambo ambalo linaweza kumfanya ashindwe kupata usingizi, kwa sababu ya mawazo,”alisema Dk Slaa.

Alisema kama mtu anataka kugombea nafasi hiyo anapaswa kukumbuka maneno ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kuwa mtu anayekimbilia Ikulu anapaswa kuogopwa kama ukoma.

Alisema mtu wa aina hiyo mara nyingi anakusukumwa na maslahi binafsi kuliko maendeleo ya watu.

Dk Slaa alisema maendeleo yanapatikana bila ya hata kuingia ikulu na kwamba la msingi ni viongozi kujipanga katika kupigania maendeleo ya wananchi.

Alisema mkakati wake ni kuhakikisha kuwa wananchi wa Karatu wananufaika na uongozi wake kwa kuwatafutia maendeleo na kuwaondolea kero kama ya maji na kadhalika.

Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na uvumi kwa Dk Slaa ana mpango wa kuwania kiti cha urais kupitia tiketi ya Chadema.

Kwa mujibu wa habari hizo, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, hana mpango wa kuwania tena nafasi hiyo na badala yake anakwenda kuwania ubunge katika Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro.

Tags:

0 comments

Post a Comment