Maelfu ya mashabiki walimiminika Khartoum |
Maelfu kwa maelfu ya mashabiki kutoka Misri na Algeria walimiminika jijini Khartoum huku wakipeperusha bendera zao za kitaifa.
Kulikuwa na wasiwasi mkubwa kiasi cha serikali ya Sudan kuwatuma askari elfu 15 kuwatenganisha mashabiki wa timu hizo na kudhibiti usalama.
Wengi walikuwa wakiisubiri mechi hiyo kwa hamu kubwa kutokana na uhasama kati ya timu zote.
Mashabiki wa timu hizo walipigana wakati wa mechi ya marudio jijini Cairo, Misri.
Timu zote zilimaliza mechi zao za kufuzu kwa pointi na mabao sawa, hali ambayo ilibidi FIFA kuandaa mechi ya kuamua atakayenyakua tiketi ya kuelekea kwa fainali za kombe la dunia huko Afrika ya Kusini.
0 comments