Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Ajali ya treni Urusi huenda ni bomu

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Ajali ya treni Urusi
Moja ya mabehewa yaliyopindika katika ajali ya treni Urusi
Serikali ya Urusi inachukulia ajali ya treni iendayo kasi ambapo hadi sasa watu 25 imearifiwa wamekufa huenda ni kazi ya magaidi.

Kumegunduka shimo karibu na ilipotokea ajali hali inayoibua hisia huenda bomu lilitumika kung'oa mataruma ya reli.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Urusi, mwendesha mashtaka mkuu tayari amefungua shauri kwa mashtaka ya ugaidi.

Treni hiyo ilipata ajali eneo la mashambani wakati ikisafiri baina ya Moscow na St Petersburg.

Mamia ya waokoaji na maafisa wa serikali wamekuwa wakifanya kazi usiku kucha katika eneo la ajali karibu na mji wa Bologoye katika mkoa wa Tver.

Baadhi ya ripoti zinaeleza huenda watu wanaofikia 39 wamekufa.

Treni hiyo ilikuwa imebeba zaidi ya watu 650. Zaidi ya watu 90 wamelazwa hospitalini na kuna wangine walisafirishwa kwa helikopta.

Mkuu wa shirika linalomiliki njia za reli la Russian Railways, Vladimir Yakunin, amesema wachunguzi wanaamini ajali hiyo imetokana na vitendo vya ugaidi.

Tags:

0 comments

Post a Comment