Chanjo hiyo ambayo ni mchanganyiko wa chanjo mbili zilizofanyiwa majaribio hapo awali, iligaiwa kwa watu 16,000 nchini Thailand.
Watafiti hao wamesema imepunguza kwa takriban theluthi ya hatari ya kuambukiza ukimwi, virusi vinavyosababisha ukimwi.
Imesifiwa kuwa ni hatua muhimu hasa katika nyanja ya kisayansi, licha ya kuwa chanjo hiyo bado ina safari ndefu ya kutumika duniani kote.
Utafiti huu ulifanywa na jeshi la Marekani na serikali ya Thailand kwa zaidi ya miaka saba kwa watu waliojitolea.
Watu hao waliojitolea walikuwa wanawake na wanaume wa kati ya umri wa miaka 18 hadi 30 katika maeneo yaliyoathirika sana na ugonjwa huo huko Thailand.
0 comments