Mkutano wa NATO Poland.
Wakati Marekani imewataka leo washirika wake wa NATO huko Krakau,Poland kuchangia vikosi zaidi kulinda usalama wakati wa uchaguzi wa Rais hapo August,nchini Afghanistan,washirika hao hawakuitikia ombi hilo mikonop miwili.
Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Bw.Franz Josef Jung, amepinga leo mpango wa Marekani wa kukitumiwa kikosi cha NRF cha NATO ili kusimamia usalama wakati wa uchaguzi nchini Afghanistan.
Waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates alisema
kwamba hangeomba idadi maalumu ya vikosi zaidi kuchangiwa na wanachama wa NATO wakati wa kikao cha leo. Alisema lakini kuwa Washington ingependa kuiona wanachama wanachangia kwa kipindi kifupi kijacho vikosi zaidi kutoka kile kikosi cha kutumika haraka panapozuka msukosuko-RAPID DEPLOYMENT FORCE (NRF) kwa ufupi ambacho hadi sasa bado kutumika.
Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Franz Josef Jung alisema leo huko Krakau kwamba anaupinga mpango huo wa Marekani wa kutumiwa kikosi hicho kuweka usalama wakati wa uchaguzi wa rais wa afghanistan hapo August 20.Nchi nyengine shirika za Ulaya zinafahamika kuwa n a msimamo sawa na huo .Kikiwa kimeundwa mwaka 2002 wakati wa mkutano wa kilele mjini Prague,Jamhuri ya Czech na kutangazwa tayari kufanya kazi miaka 4 baadae, NRF ni kikosi kinachokusudiwa kulipa shirika la ulinzi la NATO msaada haraka unapohitajika ukijumuisha vikosi tangu vya wanamaji,vya aridhini na hata vya wanahewa na chernye uwezo wa kutumika baada ya kutolewa ilaani ya siku 5 tu tena popote pale ulimwenguni.
Lakini kutoafikiana juu ya jukumu lake na kutokuwa tayari kabisa kwa wingi wa wanachama kuchangia vikosi kumeweka pingamizi katika matumizi yake katika safu za mapigano.
Hadi sasa kikosi hicho kimetumika mara chache tu na hasa kwa shughuli za uomkozi za kibinadamu mfano katika ule msiba wa mafuriko wa kimbunga cha Katrina huko Marekani,2005.
Mpango wa asili wa kuwa na kikosi cha askari 25,000 umeshaachwa kabisa.Waziri wa ulinzi wa Uingereza,John Hutton aliarifu kwamba atautumia mkutano huu wa leo mjini Krakau kupendekeza kuundwa kwa kikosi cha askari 3000 cha kuwa tayari kikiwa na jukumu la kulinda ardhi ya nchi za NATO indapo ikihujumiwa.Raia hii ni kuzitoa wasi wasi nchi za ulaya ya mashariki zanachama wa NATO kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Georgia August mwaka jana pamoja na kutoa msaada zaidi kwa Afghanistan.
Waziri huyo wa uingereza amesema kikosi cha aina hii chaweza pia kikazima ubishi uliozuka juu ya matumizi ya kikosi cha NRF.
Rais barack Obama wa Marekani ameidhinisha kupelekwa askari 17.000 zaidi nchini Afghanistan wiki hii na hii itafanya jumla ya askari wake huko kuwa 55,000.Hii itaongezea askari 30.000 waliopo huko kutoka nchi 40 nyenginezo nyingi zikiwa wanachama wa NATO.
Baadhi ya nchi za ulaya zimetangaza mipango ya kupeleka Afghanistan askari zaidi lakini idadi yao haizidi mamia na sio maalfu na Ujerumani inadai kikosi cha NRF kamwe kisitumike Afghanistan kwa shughuli kama hiyo ya kusimamia usalama wakati wa uchaguzi.
Marekani imefadhahishwa na kusitasita kwa washirika wake wa Ulaya kujitolea kupeleka Afghanistan vikosi vyao zaidi tena kwa muda mrefu na hasa upande wa kusini mwa Afghanistan ambako changamoto dhidi ya watalibani ni kali mno.Kikao cha leo mjini Krakau,Poland kitatoa mwangaza kwa kadiri gani pande hizi mbili zitaridhiana.
0 comments