Usiku wa kuamkia leo, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam, Rais wa Jakaya alibariki sherehe za kutimiza miaka mitatu ya kikundi cha muziki nchini, Tanzania House of Talent (THT), sherehe ambazo zilienda pamoja na burudani na risala iliyosomwa na mwanamuziki Lady Jaydee kwa Rais kwa niaba ya wasanii wa Bongo Flava. Pamoja na mambo mengine, katika risala yao wasanii wameiomba Serikali iwasaidie kujenga 'Professional Mastering Studio', ombi ambalo Rais ameahidi kulitekeleza.

Mh. Rais kikwete akiwa na mwenyeji wake Ruge Mutahaba ambaye ndiye mwanzilishi wa THT.

Baadhi ya wasanii wa THT wakitoa burudani kali mbele ya Mh. Rais

Mwanadada Mwasiti, mmoja wa matunda ya THT akiimba katika sherehe hizo

Mwanamuziki Hadija Shaaban 'K-Sher', aligusa nyonyo za wageni waalikwa wakati akiimba wimbo wa Tunalia ambao unalaani mauaji ya albino nchini Tanzania na unamtaka Rais kuchukua hatua kwani ni jukumu lake. Anayemtunza ni Mbunge wa Kuteuliwa Mh. Al-Shymaa Kwegyir

Mama Salma nae alishindwa kujizui na kwenda kumtunza K-Sher.

Bi. Mwanvita Makamba wa kitengo cha Vodacom Foundation (kushoto) Fina Mango na kulia kabisa ni Meneja Masoko wa Vodacom, Ephrahim Mafuru, wakifuatilia burudani iliyokuwa akitolewa na wasanii wa THT

Lady Jaydee akisoma risala kwa niaba ya wasanii wa Bongo Flava nchini.

Ni wakati wa maakuli, Mh. Rasi akijisevia msosi wake

..mama Salma nae akijisevia kiasi chake...

Ruge akifuatiwa na Lady Jaydee katika foleni ya maakuli.

Wasanii Chid Benz (shoto) na Banana Zoro katika foleni ya chakula.

Mh. Rais na viongozi wengine wa Serikali na makampuni nchini, wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa Bongo Flava na wadau wake.
0 comments