SERIKALI imetoa muda wa siku saba kwa Mwenyekiti wa Kampuni ya IPP, Reginald Mengi kuthibitisha kwamba, kuna waziri serikalini ambaye anafanya njama za kutaka kummaliza kibiashara kwa kumbambikia kodi kubwa ili ashindwe kulipa na baadaye afilisiwe.
Mengi alitoa tuhuma hizo Jumatano wakati alipozungumza na waandishi wa habari, akidai kuwa mbali na kufanyiwa njama za kubambikiwa kodi, pia anatishia kuuawa na watu aliodai kuwa ni mafisadi. Bila ya kutaja jina, Mengi alieleza kuwa waziri anayefanya njama hizo ni kijana, lakini serikali imehamaki haraka baada ya mmoja wa wajumbe wa Baraza la Mawaziri kushushiwa tuhuma hizo nzito, ambazo kama zikithibitishwa itakuwa ni kashfa kubwa dhidi ya serikali ya awamu ya nne.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, mmoja wa mawaziri vijana katika baraza la mawaziri wa serikali ya awamu ya nne, alisema kama Mengi atashindwa kuthibitisha hilo, serikali itamchukulia hatua, zikiwepo za kutaka kusababisha uvunjifu wa amani nchini.
“Hizi ni tuhuma kali… Unapoituhumu serikali na unapomtuhumu waziri, ni lazima uwe na uthibitisho,” alisema Masha akifafanua:
“Siyo tu aendelee kueleza hivi hivi tu, aje na amseme waziri huyo ni nani; na aje na ushahidi. Asipothibitisha, tutamchukulia hatua.” Alisema maelezo ya Mengi yanachochea hisia kwa jamii kwamba, serikali inaweza kupanga mkakati wa kumwonea mtu.
“Uhuru wa vyombo vya habari si kuvitumia kutangaza vitu ambavyo vinaleta athari katika jamii, hivyo tutaliangalia suala hilo na mimi kama waziri ninayesimamia usalama ndani ya nchi, ninawajibika moja kwa moja katika jambo hili,” alisema Masha.
Alisisitiza kuwa, serikali haina mpango wa kuingilia uhuru wa vyombo vya habari, lakini kamwe haiwezi kuviruhusu vitumike kujenga hisia potofu ambayo itaweza kusababisha kuvunjika kwa amani. Alielezea Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa sheria na kanuni, hivyo kama Mengi akikaidi na kutoonyesha ushirikiano katika jambo hilo basi, atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Waziri Masha, ambaye wizara yake inahusika moja kwa moja na kazi kuu ya serikali ya kusimamia usalama wa watu na mali zao, alimtaka Mengi kuwasilisha ushahidi huo moja kwa moja kwake ama kulipelekea Jeshi la Polisi ili lichunguze na kuchukua hatua zinazotakiwa. Hata hivyo, Waziri Masha, ambaye alianza kutoa tamko hilo jana alfajiri kwenye kipindi cha Jambo Afrika cha Shirika la Utangazaji (TBC), ikiwa ni saa chache baada ya kuwasili kutoka Afrika Kusini, alisema alikuwa hajaandika notisi hiyo kwa Mengi hadi jana saa 5:00 asubuhi.
Masha alisema kuwa, kama atabainika kweli kuna waziri mwenye mpango huo, atachukuliwa hatua ili kudhihirisha kuwa nchi inaongozwa kwa utawala wa sheria. Mengi pia aliwaambia waandishi kuwa kuna watu wasiojulikana ambao walimtumia ujumbe mfupi wa maneno wenye maelezo ya kumtishia maisha, Masha alisema tayari tukio hilo limeripotiwa polisi, ambao wanalishughulikia kikamilifu na kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua.
Mengi hakupatikana jana kuzungumzia agizo hilo na ilidaiwa kuwa alikuwa akihudhuria mkutano. Hii si mara ya kwanza kwa Mengi kuingia kwenye mzozo na wanasiasa katika serikali za awamu ya tatu na ya nne. Hivi karibuni, Mengi pia aliwahi kueleza kuwa alitishiwa maisha na hivyo kupewa ulinzi mkali.Serikali yampa Mengi siku saba Leon Bahati na Peter Edson
SERIKALI imetoa muda wa siku saba kwa Mwenyekiti wa Kampuni ya IPP, Reginald Mengi kuthibitisha kwamba, kuna waziri serikalini ambaye anafanya njama za kutaka kummaliza kibiashara kwa kumbambikia kodi kubwa ili ashindwe kulipa na baadaye afilisiwe.
Mengi alitoa tuhuma hizo Jumatano wakati alipozungumza na waandishi wa habari, akidai kuwa mbali na kufanyiwa njama za kubambikiwa kodi, pia anatishia kuuawa na watu aliodai kuwa ni mafisadi. Bila ya kutaja jina, Mengi alieleza kuwa waziri anayefanya njama hizo ni kijana, lakini serikali imehamaki haraka baada ya mmoja wa wajumbe wa Baraza la Mawaziri kushushiwa tuhuma hizo nzito, ambazo kama zikithibitishwa itakuwa ni kashfa kubwa dhidi ya serikali ya awamu ya nne.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, mmoja wa mawaziri vijana katika baraza la mawaziri wa serikali ya awamu ya nne, alisema kama Mengi atashindwa kuthibitisha hilo, serikali itamchukulia hatua, zikiwepo za kutaka kusababisha uvunjifu wa amani nchini.
“Hizi ni tuhuma kali… Unapoituhumu serikali na unapomtuhumu waziri, ni lazima uwe na uthibitisho,” alisema Masha akifafanua:
“Siyo tu aendelee kueleza hivi hivi tu, aje na amseme waziri huyo ni nani; na aje na ushahidi. Asipothibitisha, tutamchukulia hatua.” Alisema maelezo ya Mengi yanachochea hisia kwa jamii kwamba, serikali inaweza kupanga mkakati wa kumwonea mtu.
“Uhuru wa vyombo vya habari si kuvitumia kutangaza vitu ambavyo vinaleta athari katika jamii, hivyo tutaliangalia suala hilo na mimi kama waziri ninayesimamia usalama ndani ya nchi, ninawajibika moja kwa moja katika jambo hili,” alisema Masha.
Alisisitiza kuwa, serikali haina mpango wa kuingilia uhuru wa vyombo vya habari, lakini kamwe haiwezi kuviruhusu vitumike kujenga hisia potofu ambayo itaweza kusababisha kuvunjika kwa amani. Alielezea Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa sheria na kanuni, hivyo kama Mengi akikaidi na kutoonyesha ushirikiano katika jambo hilo basi, atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Waziri Masha, ambaye wizara yake inahusika moja kwa moja na kazi kuu ya serikali ya kusimamia usalama wa watu na mali zao, alimtaka Mengi kuwasilisha ushahidi huo moja kwa moja kwake ama kulipelekea Jeshi la Polisi ili lichunguze na kuchukua hatua zinazotakiwa. Hata hivyo, Waziri Masha, ambaye alianza kutoa tamko hilo jana alfajiri kwenye kipindi cha Jambo Afrika cha Shirika la Utangazaji (TBC), ikiwa ni saa chache baada ya kuwasili kutoka Afrika Kusini, alisema alikuwa hajaandika notisi hiyo kwa Mengi hadi jana saa 5:00 asubuhi.
Masha alisema kuwa, kama atabainika kweli kuna waziri mwenye mpango huo, atachukuliwa hatua ili kudhihirisha kuwa nchi inaongozwa kwa utawala wa sheria. Mengi pia aliwaambia waandishi kuwa kuna watu wasiojulikana ambao walimtumia ujumbe mfupi wa maneno wenye maelezo ya kumtishia maisha, Masha alisema tayari tukio hilo limeripotiwa polisi, ambao wanalishughulikia kikamilifu na kwamba watakaobainika watachukuliwa hatua.
Mengi hakupatikana jana kuzungumzia agizo hilo na ilidaiwa kuwa alikuwa akihudhuria mkutano. Hii si mara ya kwanza kwa Mengi kuingia kwenye mzozo na wanasiasa katika serikali za awamu ya tatu na ya nne. Hivi karibuni, Mengi pia aliwahi kueleza kuwa alitishiwa maisha na hivyo kupewa ulinzi mkali.
0 comments