Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Obama 'rais mteule wa Marekani'

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Rais mteule wa Marekani, Barack Obama.
Bw Obama amempiga mweleka mpinzani wake John McCain kwa kishindo kikubwa.
Barack Obama, mgombea kupitia chama cha Democrat, amechaguliwa kuwa rais mteule wa Marekani, akiwa ni mweusi wa kwanza katika historia ya taifa hilo kubwa duniani.Kwa mujibu wa matokeo ya awali.

Anakadiriwa kuwa ameshinda kura za kutosha kumhakikishia ushindi wa kumbwaga hasimu wake John McCain wa chama cha Republican.Bw Obama amepata viti 306 kati ya 538, vya wajumbe wa kumchagua rais - electoral votes.

Mpaka matokeo hayo yakitangazwa alikuwa ameshinda idadi kubwa ya majimbo yaliyochukuliwa na chama cha Democrat mwaka 2004, pamoja vile vile Bw Obama ameshinda majimbo matatu ya Republican.

Matokeo katika majimbo mengine yasiyoegemea upande wowote bado yalikuwa hayajatangazwa.

Habari zaidi zitafuatia punde.

Tags:

0 comments

Post a Comment