Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - MVUTANO KATI YA RUSSIA NA UMOJA WA ULAYA

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

Mkutano baina ya Umoja wa Ulaya na Urusi

Urusi na Umoja wa Ulaya zitaanza tena mazungumzo juu ya ushirikiano.

Wiki iliyopita Urusi ilitangaza kuwa itaweka makombora Kaliningrad ili kukabili inachoita kuwa ni hatari inayotokana na uamuzi wa Marekani juu ya kuweka makombora ya kujihami nchini Poland na katika jamhuri ya Chek.

Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa anaeuongoza Umoja wa Ulaya kwa sasa ameitaka Urusi ikubali kufanya mazungumzo juu ya usalama wa Ulaya kabla ya kuweka makombora karibu na mipaka ya nchi za Ulaya magharibi.

Rais Sarkozy amesema hayo leo mjini Nice baada ya mkutano baina ya viongozi wa Umoja wa Ulaya na Urusi.

Akizungumza kwenye mkutano na wandishi habari katika wa Nice nchini Ufaransa rais Sarkozy alisema kuwa rais Dmitry Medvedev wa Urusi ametoa mwitikio mzuri juu ya pendekezo hilo.

Rais Sarkozy wa Ufaransa anaeuongoza Umoja wa Ulaya kwa sasa amefahamisha kuwa mazungumzo hayo yanaweza kufanyika kati kati ya mwaka ujao.

Marais hao walizungumza na wandishi habari baada ya mkutano baina ya viongozi wa Umoja wa Ulaya na Urusi ambapo pande mbili hizo zilijadili masuala ya ushirikiano,usalama na mgogoro wa fedha.

Hatahivyo rais Dmitry Medvedev amezitaka nchi za Ulaya magharibi ziwe na subira juu ya suala hilo. Amezitaka nchi hizo ziepuke kuchukua hatua za upande mmoja kabla ya kufikiwa makubaliano juu ya kuweka msingi wa usalama barani Ulaya.

Juu ya uhusiano baina ya Urusi na nchi za Umoja wa Ulaya rais wa tume ya Umoja huo Jose Manuel Barosso amefahamisha kuwa mazungumzo juu ya ushirikiano kati ya pande mbili hizo yataanza tena baada ya kusimamishwa hivi karibuni kutokana na vita baina ya Urusi na Georgia.

Mazungumzo hayo yalianzishwa mwaka jana kwa lengo la kuleta ushirikiano mkubwa zaidi katika sekta za uchumi,usalama na sheria.

Kwenye mkutano wao mjini Nice rais Sarkozy wa Ufaransa mwenzake wa Urusi Medvedev pia walijadili mgogoro wa fedha ulioikumba dunia.

Viongozi hao wametoa mwito juu ya kuleta mageuzi makubwa katika taasisi muhimu za fedha duniani. Rais Medvedev ameilaumu Marekani kwa mgogoro huo wa fedha na amesema kuwa nchi yake inataka mabadiliko yafanyike katika taratibu zinazotumika kwenye taasisi za fedha ili kuweza kupunguza usemi mkubwa wa nchi za magharibi kwenye taasisi hizo.

Marais Sarkozy wa Ufaransa na Medvedev wa Urusi wanatarajiwa kuwasili mjini Washington kuhudhuria mkutano wa nchi 20, utakaofanyika kesho ,kujadili msukosuko ulioyakumbuka masoko ya fedha duniani.

Tags:

0 comments

Post a Comment