Vita vyazuka upa mashariki mwa Kongo. |
Mapigano hayo yametokea ndani na pembeni mwa mji wa Rwindi, kiasi cha kilometa 125 kaskazini mwa mji wa Goma, jimbo la Kivu ya Kaskazini.
Mapigano hayo yamezuka licha ya Jenerali Nkunda kunukuliwa akisema atakubali majeshi yake kuweka silaha chini iwapo serikali nayo itaheshimu hayo.
Alitoa tamko hilo wakati alipozungumza na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa mzozo wa Kongo, Olusegun Obasanjo.
Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la kutunza amani la Umoja wa Mataifa Kanali Jean-Paul Dietrich haijafahamika bado idadi ya watu waliokufa au kujeruhiwa katika mapigano hayo yaliyoanza siku ya Jumapili.
0 comments