You Are Here: Home - - Mh. Balozi JAKA MWAMBI, BALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MOSCOW - RUSSIA
IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
muda mfupi baada ya Mh. Jaka Mwambi kukubaliwa rasmi na Rais wa Russia Dmitry Medvedev kuwa Balozi wa Tanzania Moscow - Russia, kulifanyika hafla fupi katika ubalozi wa Tanzania Moscow, Katika hafla hiyo, Mh. Balozi alitoa Hotuba yake ambayo sehemu kubwa iliwalenga zaidi wanafunzi wanaosoma hapa kwa kuahidi kushirikiana na wanafunzi (kila mwanafunzi ka nafasi yake) katika kutatua tatizo lolote litakalojitokeza kwa njia ya majadiliano. Aliendelea kusema kuwa anawachukulia wanafunzi kama watoto wake (akawataja majina) na angependa kuishi nao hapa kama jamii moja ya watanzania, jinsi anavyoishi na watoto wake. Katika hotuba yake hiyo Mh. Balozi alionesha masikitiko yake kwa mambo yaliyojitokeza na kuahidi kuwa atashirikiana kwa nguvu zake zote katika kutatua matatizo ya wanafunzi kwa njia ya mazungumzo. Akaendelea kusema kuwa asingependa mambo kama yaliyotokea kwa wanafunzi kugoma Ubalozoni yarudiwe tena na kutoa msimamo wake kuwa atafanya awezalo ili mambo kama hayo yafutike katika akili ya watanzania. Mh. Balozi hakuacha kusema ukweli juu ya baadhi ya viongozi wanatumia uongozi wao vibaya kwa kuonesha kuwa wanaweza kupambambana ili wapendwe au kusalia kwenye uongozi wao. Mbali na hayo Mh. Balozi aliwaasa wanafunzi kusoma kwa bidii ili kupata elimu bora na mara baada ya elimu angependa sana kama wanafunzi hao wangerudi nyumbani na kuliendeleza Taifa letu Tanzania. Katika hafla hiyo pia walihudhuria wageni wengine (watanzania na wasio watanzania) ambapo Mh. Balozi aliwaasa Watanzania tulifikirie zaidi Taifa letu na tujitahidi kwa namna yoyote ile kuhakikisha nchi yetu inainuka kiuchumi. Hafla ambayo ilihudhuria na watu mbalimbali ikiwa ni pamoja na wawakilishi wa makundi mbalimbali ya watanzania wanaoishi hapa Russia. kwa upande wa TSU alihudhuria makamu mwenyekiti Linda Jonathan, Umoja wa africa ASSAFSTU alihudhuria makamu katibu Assenga Boniface na upande wa tawi la CCM alihudhuria mwenyekiti Dr. Alifred Kamuzora.
mii namwombea mungu Balozi wetu ili aweze kutenda yale yaliyokusudiwa. Amen
mheshimiwa wetu tunakutakia kila la kheri takita kufanikisha zoezi hili la uongozi