Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - kashfa ya RICHMOND, watu walizwa.....

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter Miongoni mwa vigogo hao ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU, Bw. Edward Hosea, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Johnson Mwanyika na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Arthur Mwakapugi. Wengine ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa TAKUKURU, Bw. Alex Mfungo na maofisa wengine wanane wa taasisi hiyo waliochunguza mkataba huo wa Richmond. Maofisa hao wanane wa TAKUKURU ni wale ambao awali waliuchunguza mkataba huo \'feki\' na kutoa majibu wakiufagilia kuwa ni mzuri usiokuwa na mazingira ya rushwa. Hata hivyo Waziri Pinda amesema kutokana na nafasi aliyonayo kikatiba Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mwanyika, suala lake linashughulikiwa na Ofisi ya Rais, Ikulu. Akizungumzia mawaziri wawili waliojiuzulu, Bw. Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha, Waziri Mkuu Pinda amesema licha ya kujiuzulu kwao, bado vyombo vya dola vinaendelea kuwachunguza ili Serikali iweze kujiridhisha kuwa hawakufanya makosa ya jinai kama vile kupokea rushwa. Waziri Mkuu Pinda amesema ikiwa vyombo vya dola vitabaini kuwa mawaziri hao walifanya makosa ya jinai, hatua za kisheria zitachuliwa dhidi yao.
Tags:

0 comments

Post a Comment