Pages

Thursday, April 14, 2011

Ouattara aahidi kuleta haki Ivory Coast


Rais mpya wa Ivory Coast Alassane Ouattara amesema pande zote zilizohusika katika ghasia lazima zishtakiwe.
Alisema ataiomba mahakama ya kimataifa ya uhalifu kufanya uchunguzi juu ya mauaji ambapo majeshi yake na ya mpinzani wake Laurent Gbagbo yanahisiwa kuhusika.
Bw Gbagbo alikamatwa siku ya Jumatatu na majeshi ya Bw Ouattara baada ya kukataa kuwa alishindwa kwenye uchaguzi wa mwezi Novemba.
Bw Ouattara alisema, sasa atakabiliwa na mashtaka "katika kiwango cha kitaifa na cha kimataifa."
Katika mkutano uliofanyika kwenye mji wa kibiashara wa Abidjan, Bw Ouattara alisema Bw Gbagbo amepelekwa eneo salama.

No comments:

Post a Comment