Wachunguzi wa uchaguzi nchini Tanzania wamesema hakuna taarifa yoyote kuu ya dosari iliyojitokeza inayoweza kuathiri matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya Jumapili.
Kiongozi wa jopo la wachunguzi kutoka Jumuiya ya Madola Bw Paul East, amesema uchaguzi huo uliendeshwa vyema ikilinganishwa na ya miaka mitano iliyopita.
Hata hivyo East amesema kuchapishwa kwa matokeo ya uchaguzi huo kumecheleweshwa sana.
Amesema kutokana na kuwepo teknolojia ya kisasa, haipaswi matokeo hayo ya uchaguzi kuchukua siku nne hata tano kuweza kujulikana.
Wakati huo huo Mawaziri kadhaa tayari wamepoteza viti vyao vya ubunge katika uchaguzi huo.
0 comments