Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Mkutano wa viongozi wa Ufaransa, Ujerumani, Urusi.

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter Viongozi wa Ufaransa, Ujerumani na Urusi wanakutana leo, katika jitihada za kuimarisha uhusiano wao na kutafuta msimamo wa pamoja kuhusiana na mpango wa Jumuiya ya kujihami ya NATO, wa kuwa na mfumo wa kujilinda na makombora. Ni mpango Urusi inaona kama tishio. Suala la usalama ni kikwazo kikubwa kwa uhusiano kati ya Urusi na mataifa ya Magharibi na utakuwa ajenda kuu katika mkutano huo kati ya Marais Nicholas Sarkozy Dmitry Medvedev na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel. Mkutano huo unafanyika katika mji wa Deauville Ufaransa, kabla ya mkutano wa NATO mjini Lisbon, Ureno mwezi ujao. Ingawa Marekani na Jumuiya ya NATO wanashikilia kuwa mpango huo ni wa kujilinda dhidi ya vitisho vya makombora kutoka Iran, wasiwasi wa Urusi ni kuwa mpango huo huenda ukatumiwa dhidi ya silaha zake za masafa marefu na kuudhoofisha uwezo wake wa kuzuia mashambulizi.
Tags:

0 comments

Post a Comment