You Are Here: Home - - Waziri Mkuu wa Iraq aiomba Iran usaidizi.
IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Katika ziara yake nchini Iran, Waziri Mkuu wa Iraq, Nuri al-Maliki ameitaka nchi hiyo, kusaidia kuijenga upya Iraq, iliyozongwa na vita, huku mahasimu wake wakiishutumu Jamhuri hiyo ya Kiislamu kwa kuingilia mambo ya ndani ya Iraq. Ziara ya siku moja ya Al-Maliki, Iran, inanuia kutafuta uungwaji mkono katika jitihada zake za kupata muhula wa pili baada ya uchaguzi wa Machi 7 kushindwa kupata mshindi nchini humo. Vyombo vya habari nchini Iran viliripoti kuwa al-Maliki alikutana na viongozi wa ngazi ya juu akiwemo Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei. Katika mkutano wake na Khamenei, al-Maliki alisema uhusiano wa Iraq na majirani zake ni muhimu katika ujenzi wa nchi hiyo iliyokumbwa na vita vya miaka minane na Iran, uongozi wa kimabavu wa Saddam Hussein na uvamizi uliongozwa na Marekani kumuondoa madarakani Saddam Hussein. Kwa upande wake Khamenei alimuambia al-Maliki kuwa matatizo ya Iraq yanatokana na kuwepo kwa majeshi ya Marekani nchini humo.
0 comments