Takriban watu 13 walizama na wengine wanane hawajulikani walipo baada ya manowari ya kijeshi ya Marekani yalipojaribu kusaidia mashua nyepesi ndogo tena nyembamba iliyoharibika kwenye ghuba ya Aden.
Maafisa wa manowari hayo ya kijeshi mjini Washington walisema USS Winston Churchill ilijaribu lakini ilishindwa kurekebisha injini ya mashua hayo mepesi.
Ikaanza tena kuyavuta manowari hayo pwani ya Somalia.
Lakini jitihada za uokoaji zilibadilika na kuwa balaa wakati abiria walipokimbilia upande mmoja wa chombo hicho kupata chakula na misaada, na kusababishia ipinduke.
Abiria wote 85 walirushwa kwenye maji, japo wengi wao waliokolewa.
Jeshi hilo la majini la Marekani lilikuwa na Waethiopia 75 na Wasomali 10, na boti hiyo ilikuwa ikitokea Somalia.
Uchunguzi
Boti hiyo mwanzo iligunduliwa katika ghuba ya Aden siku ya Jumapili.
Baada ya mabaharia kutoka kwenye manowari kushindwa kurekebisha injini ya mashua hayo madogo, walianza kukivuta chombo hicho pwani ya Somalia.
Abiria 61 waliokolewa na kwa sasa wako kwenye meli ya USS Churchill, lakini 13 walizama na wanane hawajulikani walipo.
Jeshi hilo lilisema bado linafanya uchunguzi kujua kitu gani kilitokea.
Haijajulikana wazi kwanini mashua hayo yalikuwepo eneo hilo, njia inayopita meli nyingi iliyokumbwa na mashambulio na maharamia wa Kisomali.
Lakini Umoja wa Mataifa umesema takriban Waafrika 74,000- zaidi kutoka Ethiopia na Somalia- walivuka ghuba ya Aden kuelekea Yemen mwaka 2009 wakikimbia umaskini na migogoro.
0 comments