Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Wamisri walio na wake wa Kisrael kupoteza uraia

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

Wamisri walio na wake wa Kisrael kupoteza uraia

Raia wa Misri wakiipiga viatu bendera ya Israel
Raia wa Misri wakiipiga viatu bendera ya Israel
Mahakama ya Kiutawala nchini Misri imeunga mkono uamuzi wa mahakama unaoagiza wanaume raia wa Misri waliowaoa wanawake wa Kisrael kupoteza uraia wao.
Jaji katika mahakama kuu alisema wizara ya mambo ya ndani lazima itoe maelezo kwa baraza la mawaziri kuhusu wanaume wote raia wa Misri waliowaoa Wayahudi na WaIsraeli wenye asili ya Kiarabu.
Kila kesi itazingatiwa kivyake,lakini baadaye hatua zinaweza kuchukuliwa kuwanyang'anya uraia wao, na hata ule wa watoto wao.
Wakili aliyewasilisha kesi hiyo, alisema watoto wanaozaliwa katika ndoa kama hizo wasiruhusiwe kujiunga na jeshi.
Alisema lengo lake ni kuwahifadhi vijana wa Misri na usalama wa taifa.
Kusiwe na kizazi kipya "ambacho hakitokuwa mtiifu kwa Misri na ulimwengu wa Kiarabu" alisema wakili huyo.
Hakuna rufaa inayoweza kukatwa kupinga hukumu hiyo, na uamuzi wa sasa unathibitisha na kuunga mkono hukumu uliyotolewa na mahakama ya ngazi ya chini mwaka uliopita.
Awali serikali ilikata rufaa dhidi ya uamuzi huo, ikisema ni bunge tu lenye uwezo wa kuamua juu ya masuala kama hayo.
Tangu mwaka wa 1979 baada ya Misri kuwa nchi ya kwanza ya Kiarabu kutia saini mkataba wa amani na Israel, raia wengi wa Misri wamehamia huko wakitafuta kazi na wakaowa wanawake raia wa Israel.
Tags:

0 comments

Post a Comment