Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Wanajeshi wa Israel waingia ndani ya meli ya Ireland.

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
 

Maandamano katika miji mingi duniani yafanyika kupinga hatua ya Israel ya kuzuia meli kuelekea Gaza.

 
Jeshi la Israel limesema wanajeshi wake wameingia ndani ya meli ya misaada ya Ireland inayoelekea Gaza baada ya kuizuia katika eneo la mpaka wa majini wa kimataifa. Msemaji wa jeshi hata hivyo amesema hakukuwa na mvutano na kulikuwa na ushirikiano kutoka kwa mabaharia na abiria.
Awali wanajeshi wa Israel walikuwa wametishia kuingia katika meli hiyo inayosafirisha misaada na wanaharakati ikiwa haingebadilisha mkondo wa kuelekea Gaza.Wanajeshi wa Israel washika doria kulidhibiti eneo la ukanda wa Gaza.Wanajeshi wa Israel washika doria kulidhibiti eneo la ukanda wa Gaza.
Mapema wiki hii watu tisa waliuawa wakati wanajeshi wa Israel walipoingia katika meli ya Uturuki iliyokuwa imebeba misaada kwa ajili ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.
Jana kulikuwa na maandamano katika nchi za Kiarabu yakiitaka Israel iondoe sheria ya kuzuia usafiri katika ukanda ilioanza kutekelezwa baada ya kundi la Hamas kulidhibiti eneo hilo mwezi Juni mwaka wa 2007.
Kamishna wa Umoja wa Mataifa anayesimamia haki za binaadam, Navi Pillay aliitaja hatua hiyo kuwa sio halali akisema sheria ya kimataifa inayolinda ubinadamu inapinga kuwanyima chakula raia kama mbinu ya kivita. Pillay pia alisisitiza kuanzishwa kwa uchunguzi dhidi ya uvamizi wa Israel kwa msafara wa meli hizo.
Tags:

0 comments

Post a Comment