Watu 10 Wakamatwa Marekani kwa kuipelelezea Urusi
Watu kumi wamekamatwa nchini Marekani kwa kushukiwa kuwa majasusi wa Urusi.Watu hao walikamatwa kwenye msako uliofanyika katika miji ya NewYork, Boston, New Jersey na Virginia. Mshukiwa mwingine angali anasakwa.
Idara ya Sheria ya Marekani imetoa stakabadhi kudhibitisha kuwa watu iliowazuilia wamekuwa wakikusanya habari za kijasusi a kuzipokeza kwa serikali ya Urusi.
Idara hiyo inasema baada ya uchunguzi wa muda mrefu imewanasa watu hao wakiwemo wanaume wanne na wake zao ambao wamekuwa wakifanya kazi kichichini ili kupata habari muhimu kutoka kwa ofisi za serikali na idara zingine muhimu.
Maafisa hao wa marekani pia wanasema washukiwa hao wamekuwa wakiwasajili watu wengine kwa kazi hiyo ya kijasusi. Mmoja wao anadai kuwa alikuwa ametumwa kuchunguza hasa jinsi serikali ya Rais Obama inavyoiona Urusi kabla ya rais huyo wa Marekani kuzuru urusi.
Habari hizi zimeitia serikali ya Marekani wasiwasi hasa kwa sababu rais Obama amekuwa akijaribu kuoberesha uhusiano wa serikali hiyo na Urusi.
Matukio haya yanarudisha kumbukumbu ya vita baridi kati ya mataifa hayo ambavyo vilidumu kwa zaidi ya miongo mitatu.
Katika miaka ya 60 hadi ile ya 80 karibu ulimwengu mzima ulijipata umenaswa katika vita hivyo baridi na matai. Mataifa hayo mawili yalikuwa yanang'aninia kuwa na ushawishi na hata udhibiti wa karibu mataifa yote duniani.
Na ili kufanikisha kampeni zao serikali ya Marekani na ile ya muungano wa Usovieti ziliwaweka majasusi karibu kote duniani. Na sasa takriban miaka 20 tangu vita hivyo kukoma mbinu hizo hizo bado zinaendelea kutumiwa.
0 comments