MBUNGE wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela jana alichafua hali ya hewa ndani ya ukumbi wa Bungeni baada ya kuwashukia watu aliodai wanamchezea mchezo mchafu jimboni kwake na serikali imekaa kimya. Kilango ambaye alikuwa mchangiaji wa kwanza katika hotuba ya Waziri Mkuu kuhusu makadirio ya matumizi katika bajeti ya 2010/11 alimnyooshea kidole moja kwa moja, Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo George Mkuchika kuwa amekuwa kimya mno ili hali yeye akiumizwa. Anatoa anatoa kauli hiyo wiki moja baada ya yeye na wabunge wenzake wa CCM kutaka kuonana na Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete ili waweze kumueleza malalamiko yao kwa kile wanachodai kufanyiwa hujuma katika majimbo yao. Wabunge hao ambao wiki iliyopita walikuwa na kikao cha chama katika Ukumbi wa zamani wa Bunge wa Pius Msekwa chini ya Mwenyeti wake Waziri Mkuu, Mizengo Pinda walisema wanataka kuonana na Mwenyekiti huyo kwakuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba ameshindwa kuwatatulia matatizo yao. Katika mkutano huo ulioanza saa 5.30 asubuhi, wabunge hao walisema kuwa wana ushahidi wa mchezo mchafu wanaofanyiwa majimboni kwao kwa lengo la kuwaangamiza ili waweze kutetea tena viti vyao, lakini wanaopomplekea ushahidi huo Katibu Mkuu amekuwa hashughulikii kitendo ambacho wanahisi kwamba (Makamba) yuko pamoja nao. Jana mbunge huyo alimtaka Makamba kutoa tamko kali la kukemea watu wanaingia Same Mashariki kwa kusema kuwa wametumwa kumng’oa. “Mimi namshangaa huyu Mkuchika, kuna baadhi ya magazeti yakifanya kosa kidogo yanafungiwa wakati mengine yanatutukana sana, lakini amekuwa kimya, hapa naomba Waziri Mkuu uliangalie suala hilo,” alisema Kilango. Bila kuwataja majina wamiliki wa magazeti hayo, Kilango alisema wapo ndani ya ukumbi wa bunge na akasema wamekuwa wakigawa bure magazeti hayo hadi katika jimbo lake. “Magazeti hayo ni ‘Tazama’ na ‘Mkakati’ yanatolewa bure na hadi kule Same Mashariki juu ya milima yanapandishwa kwa malori ili wananchi wayapate, hii ni kuchezea amani ya nchi mheshimiwa Waziri Mkuu, na amani ikichezewa hatuatakuwa salama,” alisisitiza. Katika hotuba yake Kilango alimtaka Waziri Mkuu kutoa tamko la wenye magazeti hayo kujitukana wenyewe kwani kwa kawaida yao wamekuwa wakitukana wenzao ili hali wao hawajitukani hali inayoonyesha kuwa wana ajenga ya siri juu ya wapambanaji wa mafisadi. Alisema katika magazeti hayo kumekuwa na picha yake ambayo siku zote inaunganishwa na mtu ambaye pembeni kunakuwa na picha ya mke wa kiongozi mkubwa wa nchi jambo linaloonyesha kuwa wanatumia migongo ya wakubwa katika kujitafutia umaarufu. Alisema mtu huyo siku zote hawezi kusimama peke yake kwa kuwa ni mbovu wa mbavu, kiuno, ndiyo maana anawatumia viongozi wakubwa ili wambembe. Katika magazeti hayo alisema pamoja na yeye Kilango lakini yamekuwa yakiwandika pia Samuel Sitta (Urambo Mashariki), Mudhihiri Mudhihiti (Mchinga), Harison Mwakyembe (Kyela). “Jimboni kwangu ni kwangu wala sio kwa Makamba ambaye wao wanasema kuwa amewatuma. Kama huyo Makamba anawatuma basi awaambie waende Bumburi huko ndiko kwake sio Same. Mbali na hilo Kilango alisema mtu yeyote atakayeingia Same Mashariki bila ya kupitia CCM atarogwa kwa kuwa chama hicho kimefamya mambo makubwa sana jimboni kwake. |
You Are Here: Home - - Kilango achafua hali ya hewa bungeni
IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
0 comments