Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Kikwete akutana na Clinton Dar

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter RAIS Jakaya Kikwete jana alifanya mazungumzo na Rais mstaafu wa Marekani, Bill Clinton, ambaye amekuja nchini kwa ajili ya kukagua shughuli zinazoendeshwa na mfuko wake unaoshughulikia upatikanaji wa huduma za afya duniani.
Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Mwandishi Msaidizi wa Habari wa Rais, Premi Kibanga, alisema kuwa akiwa katika mazungumzo na mgeni wake huyo, Rais Kikwete alimshukuru kwa mchango wake anaoutoa katika sekta ya afya nchini.

Kibanga alisema mbali na kuzungumzia mfuko huo wa Rais Clinton, viongozi hao walipata fursa ya kuzungumzia hali ya kisiasa na maendeleo ya Tanzania.

“Mchango huo wa Clinton hapa nchini ni katika masuala ya HIV/AIDS ambapo mfuko wa Bill Clinton unasaidi kutoa dawa za kupunguza makali na athari za ukimwi (ARVs),” ilisema taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Clinton amekua mstari wa mbele katika kuchangia makampuni mengi kupata nafasi ya kutengeneza dawa za ARV, jambo linalofanya dawa hizo kuuzwa kwa bei nafuu.

Taarifa hiyo ilisema kuwa mikoa ya Lindi na Mtwara imefaidika na mfuko huo kwa kuwawezesha waathirika kupata huduma za awali ikiwemo vipimo na dawa katika vituo vya maabara ya kisasa huko huko vijijini, wilayani na mikoani.

Clinton alipata wasaa wa kutembelea kituo cha Afya cha Kitere kilichoko Mtwara vijijini na kurejea jijini jioni. Anatarajia kuondoka nchini leo kwenda nchini Afrika Kusini.

Mapema jana asubuhi, Kikwete aliwaapisha Majaji 10 wa Mahakama, ambao ni John Utamwa, Samwel Karua, Beatrice Mutungi na Richard Kibela.

Wengine ni Grace Mwakipesile, Ama-Isari
Tags:

0 comments

Post a Comment