IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo inatarajia kutoa hukumu ya kesi inayomkabili Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba.
Kesi hiyo ambayo ilivuta hisia na masikio ya watu wengi wakati ikiunguruma mahakamani hapo inatarajiwa kufikia mwisho leo.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa kwa zaidi ya mwaka mmoja na kushindwa kutimiza masharti ya dhamana, hali iliyomlazimu kuendelea kukaa mahabusu.
Liyumba kwa sasa anakabiliwa na shitaka la matumizi mabaya ya ofisi ya umma, baada ya kufutiwa na mahakama hiyo shitaka la kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 221.
Shitaka hilo lilifutwa baada ya upande wa mashitaka kushindwa kudhibitisha madai yake. Katika shtaka hilo la matumizi mabaya ya ofisi, Liyumba anadaiwa kufanya mabadiliko katika mradi wa ujenzi wa majengo pacha ya BoT bila kuhusisha bodi ya wakurugenzi.
You Are Here: Home - - Hukumu ya kesi ya Liyumba leo
0 comments