Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Halmashauri Kuu CCM kukutana leo Dar

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter HALMASHAURI Kuu ya Taifa (Nec), ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), inakutana leo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Idara ya Itikadi na Uenezi ya CCM, kikao hicho ni cha kawaida na kitafuatiwa na semina ya siku mbili ya Wenyeviti na Makitibu wa Mikoa na Wilaya zote nchini ambayo itafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam kuanzia Aprili 10, mwaka huu.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa katika semina hiyo mada kadhaa zitajadiliwa miongoni mwa hizo ikiwa ni kuhusu uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa atakuwa mmoja kati ya viongozi na wakongwe wa siasa nchini ambao watatoa mada katika semina hiyo.

Pia ilielezwa kuwa semina hiyo itafuatiwa na nyingine ya siku tatu itakayofanyika mjini Dodoma na itahusisha makatibu wa siasa na uenezi wa mikoa yote nchini.
Tags:

0 comments

Post a Comment