Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - CUF yashistushwa na kauli ya Tendwa

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter CHAMA cha Wananchi (CUF), kimeeleza kumeshitushwa kwake na kauli ya Msajili wa Vyama vya Siasa John Tendwa, kuwa chombo chenye aumuzi ya mwisho kuhusu gharama za uchaguzi ni serikali na kwamba vyama vya siasa na wadau wengine ni washirikishwaji.

Taarifa iliyotolewa na Naibu Mkurugenzi wa Oganazesheni na Uchaguzi wa CUF, Sheweji Mketo, ilisema wakati akizungumza na waandishi wa habari Tendwa alisema vyovyote itakavyokuwa, gharama za uchaguzi mkuu zitakazoruhusiwa kisheria kutumiwa na vyama zitakuwa kati ya Sh. 35 bilioni na Sh 40 bilioni.

"Lakini akaongeza pamoja na ofisi yake kuvishirikisha vyama vya siasa na wadau wengine, lakini mwenye uamuzi wa mwisho kuhusu kiasi gani kupitishwe ni serikali na kwamba yeye ndiye mshauri wake mkuu," ilisema taarifa.

Hata hivyo Mketo katika taarifa yake alisema kauli hiyo ya Msaji wa Vyama vya Siasa ni ya upotoshaji na kwamba inapinga na misingi ya demokrasia.

"CUF inaamini kuwa nchi inayofuata misingi ya demokrasia na utawala bora ni ile inayothamini na kuzingatia michango ya wadau na vyama vya siasa," alisema Mkurugenzi huyo kupitia katika taarifa yake.

Alisisitiza kuwa nchi inayofuata misingi bora ya demokrasia na utawala bora ni ile inayoheshimu na kuzingatia maoni ya wadau na vyama vya siasa.

Alisema chama chak kimesikitishwa na kauli ya Tendwa na kwamba inayonyesha jinsi anavyoshiriki katika kuvuruga demokrasia na kuvifanya vyama vya siasa kuwa mihuri ya kupitisha maamuzi ya serikali ya CCM.

“Kwa hali hiyo tunamtilia kama kweli anaweza kusimamia majukumu yake bila upendeleo,”alisisitiza.
Tags:

0 comments

Post a Comment