Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - China yaikopesha Tanzania bilioni 239

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter China yaikopesha Tanzania bilioni 239 ERIKALI ya Tanzania na ile ya China zimesaini mikataba mitatu yenye jumla ya Sh 239.2 bilioni.Katika fedha hizo Sh229 bilioni ni mkopo wenye masharti nafuu na Sh13.3 bilioni ni msaada.

Mikataba hiyo imesainiwa jana Ikulu jijini Dar es Salaam na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo aliyeiwakilisha serikali ya Tanzania, na Waziri wa Biashara wa China, Chen Deming na kushuhudiwa na Rais Jakaya Kikwete pamoja na baadhi ya mawaziri wa Bara na Visiwani.

Waziri wa Fedha na Uchumi wa Zanzibar, Mwinyihaji Makame alisaini mkataba wa msaada Sh 3.8 bilioni kwa ajili ya visiwa hivyo.

Mkataba wa kwanza unahusisha msaada wa fedha kwa ajili ya ushirikiano wa kiuchumi na ufundi baina ya serikali hizo mbili, huku Bara ikipata Sh9.5 bilioni na Zanzibar Sh3.8 bilioni.

Mkataba wa pili ni mkopo wa Sh132.9 bilioni kwa ajili ya mkonga wa taifa wa mawasiliano, ikiwa ni sehemu ya pili ya utekelezaji wa uboreshaji wa sekta ya mawasiliano nchini. Katika awamu ya kwanza mwaka 2008, China ilitoa Sh93 bilioni.

Mkataba wa tatu ni mkopo wa Sh93.5 bilioni kwa ajili ya kuboresha sehemu mpya (terminal 2) ya Uwanja wa Ndege wa Zanzibar.

Akizungumza mara baada ya kusainiwa kwa mikataba hiyo, Waziri Mkullo alisema mbali na kutoa fedha hizo, China imeitaka Tanzania kuandaa nyaraka za upembuzi yakinifu kwa lengo la kuifanyia matengenezo reli ya kati.

"Tuliiomba serikali ya China itusaidie kuijenga reli ya kati. Kimsingi imekubali lakini imetutaka sasa tuandae upembuzi yakinifu kuhusu reli hiyo na tuwakabidhi. Kukubali huku ni kutokana na umuhimu wa reli hiyo," alisema Mkullo.

Naye Waziri Deming alisema serikali yake itatuma timu ya waatalamu katika masuala ya biashara, reli na bandari kabla ya Juni mwaka huu ili waweze kukutana na wenzao wa Tanzania na Zambia na kuangalia jinsi ya kuimarisha sekta hizo.

Tags:

0 comments

Post a Comment