Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Watu wa Haiti walioathirika na tetemeko la Arthi washauriwa kurudi Africa

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
SENEGAL YAWAKARIBISHA WATU WA HAITI
Rais wa Senegal Abdoulaye Wade.

RAIS wa Senegal, ametoa ardhi ya bure kwa watu wa Haiti walioathirika kwa tetemeko la ardhi ambao watakubali kurejea Afrika...


Rais wa Senegal amesema atatoa sehemu ya shamba iwe makazi kwa watu walioathirika na tetemeko la ardhi nchini Haiti.
Rais Abdoulaye Wade amesema raia wa Haiti ni watoto wa bara la Afrika kwa kuwa asili ya watu wa Haiti ni watumwa,wakiwemo wengine wanaoaminika kutokea Senegal.
"Rais anatoa fursa kwa mtu yeyote wa Haiti kurudi katika asili yake kwa hiari," amesema msemaji wa bwana Wade, Mamadou Bemba Ndiaye.
Tetemeko la ardhi lilotokea siku ya jumanne limewaua maelfu ya watu na kuwaacha wengi bila makazi.
Majengo yamebaki kuwa kifusi,watu wengi hawajapata msaada, na watu wamekuwa wakiondoka nje ya mji mkuu, Port-au-Prince.
Tags:

0 comments

Post a Comment