HAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema hakuna tatizo kwa chama hicho, kuungana na CUF na kuunda serikali ya mseto na kueleza kwamba wanaobeza jitihada hizo ni mashetani.
Akizungumza na gazeti hili, katika mahojiano maalum ofisini kwake Kisiwandui, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar Saleh Ramadhan Ferouz alisema wanaofanya hivyo, pia wana mawazo ya kikoloni.
“Mimi naweza kumwita ibilisi mkubwa au ni shetani yeyote ambaye hataki kuyaunga mkono mazungumzo haya kwa sababu ninaamini huyo, atakuwa hatutakii mema Zanzibar na anataka sisi tugombane miaka yote…mtu huyo atakuwa ananufaika na migogoro inayotokea Zanzibar,†alisema.
Ferouz alisema awali uamuzi wa rais Karume kukutana na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif ulikuwa wake mwenyewe lakini, sasa umekuwa uamuzi wa Wazanzibari wote kwa kuwa kila kiongozi amewaambia wanachama wake na wasiokuwa na vyama pia wameelezwa.
Mkutano ulifanyika Novemba 22, mwaka huu, ulitayarishwa na Chama Cha Mapinduzi na haukuwa wa serikali na pale rais alipokuja kuhutubia alikuja pale kama Makamu mwenyekiti wa CCM, hakuja kama rais na wananchi walikuja kusikiliza maelekezo ya chama. Kwa nini tuseme uamuzi ni wa rais Karume?.
Sasa hivi tatuwezi tena kuita mazungumzo ya rais Karume na Maalim Seif sasa tunayaita maridhiano ya Wazanzibari kwa sababu viongozi wetu wote wamewasilisha mazungumzo hayo kupitia mikutano ya vyama vyao,†alisema.
Alisema hakuna haja ya kutafiti kilichozungumzwa na viongozi hao wawili, lakini muhimu ni watu kufahamu dhamira ya kweli iliyopo ambayo lengo lake ni kuondoa uhasama na chuki na kujenga Zanzibar mpya yenye ushirikiano ambao faida zake, zitaonekana muda mfupi ujao.
Mimi matarajio yangu ni makubwa sana kwamba sasa tunakwenda katika kuweka historia mpya ya hapa kwetu Zanzibar,†alisema Ferouz.
Ferouz amewataka wananchi hususani wanachama wa CCM kuacha kukumbatia historia mbaya ya ukoloni ili waanze kujenga mahusiano mema yatakayoleta umoja na ushirikiano kati ya vyama hivyo viwili hasimu vya CUF na CCM.
Ferouz alisema bado kuna kundi kubwa la wananchi ambalo bado linatawaliwa na historia na kwamba kutokana na hali hiyo, kundi hilo, hawawezi kusaidia kuleta maendeleo na kwamba ushirikiano unaweza kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi.
Huwa tunaulizwa huko mitaani nyie mnawaamini hawa CUF?, wananchi wengi bado wanapenda kuwa watumwa wa historia na hilo ni jambo baya kwa nini tuendelee kuwa watumwa wa historia? alihoji Naibu Katibu mkuu huyo.
Alisema ni ukweli kwamba zamani kulikuwa na migogoro iliyochochewa na vyama vingi, lakini vyama hivyo sasa havipo tena na kamwe ukoloni hautorudi kwa kuwa mkoloni aliondolewa Zanzibar.
Aliwataka wananchi wa Zanzibar kuacha chuki na uhasama badala yake wajenge umoja ambao utaleta faida na maendeleo.
Alisema kuna watu ambao wanahisi endapo CCM itaungana na CUF watarudishwa kwenye ukoloni jambo ambalo sio sahihi kwani, vyama vya wakoloni sasa havipo wala hakuna mkoloni ambaye atathubutu kukanyaga Zanzibar kwa kuwa sasa wananchi ndio wenye kutawala.
Hatuwezi kuwa watumwa, lakini pia wapo watu wanaamini kuwa labda tutamkaribisha mkoloni hivi kweli katika karne hii kuna mkoloni atarudi Zanzibar, kweli mimi nadhani tusiwe na mawazo hayo…hapa mkoloni harudi, na tufike pahala turidhike kwamba yaliopita yameshapita sasa tujenge historia mpya ya nchi,†alisisitiza Ferouz.
Alisema CCM imekuwa ikiwaelimisha wanachama wake kuhusu suala hilo, lakini imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwamo maswali kama kutakuwepo na mfumo mwingine wa uchaguzi visiwani Zanzibar mwakani kwa kuwa wananchi wengi wanaamini kuwa hata uchaguzi ukifanywa mara ngapi hakutakuwa na mabadiliko kwa kuwa viongozi wa vyama hivyo, wameungana
0 comments