Obama kupokea tuzo ya Nobel leo | ||||
Rais Barack Obama yuko nchini Norway ambapo anatarajiwa kupokea tuzo ya amani ya Nobel katika sherehe ya kutolewa tuzo hiyo mjini Oslo. Bw Obama ameshinda tuzo hiyo kutokana na kile kamati kuu inasema kuwa juhudi zake kuimarisha uhusiano mwema duniani kwa kutumia diplomasia. Hata hivyo ushindi wa tuzo hiyo umekosolewa na baadhi ya watu ambao wanaona umekuja kwa haraka wakihoji mafanikio ya Obama katika sera ya kimataifa hata kabla ya wake wa kwanza kumalizika. Wakati huo huo sanamu ya rais Obama akiwa mtoto wa miaka kumi inazinduliwa hii leo mjini Jakarta, Indonesia. Obama awahi kuishi nchini humo utotoni wake. |
You Are Here: Home - - Obama kupokea tuzo ya Nobel leo
IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
0 comments