Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Kipa wa timu ya Ghana aliyesajiliwa Yanga akichimba biti kali...

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Kipa Mghana achimba mkwara mkali
Kipa mpya wa timu ya Yanga, Yew Berko akifanya mazoezi katika uwanja wa shule ya kimataifa ya Tanganyika (IST) jijini Dar es Salaam jana
Na Oliver Albert KIPA Mpya wa Yanga kutoka klabu ya Liberty Professionals FC ya Ghana, Yaw Berko amesema yupo tayari kuondoka ikiwa klabu hiyo itamzingua. Kipa huyo aliyezaliwa mwaka 1980, Accra, Ghana alisema amesaini kuichezea timu hiyo kwa miezi mitatu ili aweze kusoma mazingira. "Ni kweli nimesaini miezi mitatu kwa sababu kwanza nimeambiwa ligi inamalizika Machi mwakani, lakini pili nasoma uendeshaji wa klabu. "Timu za soka nazijua mambo yanakuwa mengi mno, nangoja kwanza nione viongozi, mashabiki wananichukuliaje, kama watanikubali basi nitaongeza mkataba upya na nikioona mambo yanakwenda sivyo siwezi kuendelea nao. "Nitacheza kwa miezi hiyo kisha nitarudi nyumbani Ghana na sasa itatategemea nitakavyokubalika, wakinikubali narudi nikiona hawanikubali sirudi tena,"alionya Berko, ambaye alitokea Liberty Professionals ya Ghana. Alisema amefurahia kutua katika timu hiyo kwani ina wachezaji wenye vipaji na kuongeza mazoezi ya kocha Kostadian Papic ni kiboko. Akizungumzia ushindani na makipa wenzake wa klabu hiyo ambao sasa wako wanne, Berko alisema kocha ndio ataamua. "Nimekuja kusaidiana na wenzangu, kila mmoja ni kipa mzuri hapa ingawa tunatofautiana kwa mambo kadhaa lakini nia yetu ni kuisaidia Yanga hivyo kocha ndio ataamua nani adake na katika mechi ipi," alisema Berko, ambaye katika timu yake alikuwa akivaa jezi namba 40. Kipa huyo ameonyesha kiwango kikubwa cha kupangua mashuti katika mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) Masaki jijini Dar es Salaam. Papic amemsifu kipa huyo kuwa ni mzuri kutokana na kuwa na uzoefu wa muda mrefu.
Tags:

0 comments

Post a Comment