Waziri wa Fedha wa Ugiriki, George Papaconstantinou amesema msaada wa fedha kutoka nchi za kanda ya Euro na shirika la fedha la kimataifa , IMF upo njiani lakini utachukua siku kadhaa kabla ya kufika nchini humo.
Siku ya Ijumaa, Ugiriki ilitoa ombi kwa Umoja wa Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, kuipatia msaada wa Euro bilioni 45 ili iweze kulipa madeni yake makubwa.
Lakini Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.amesema, kuna masharti ya kutimizwa. Kwanza, mpango unaoaminika kupunguza matumizi, ujadiliwe kati ya Ugiriki, Kamisheni ya Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa. Pili, mpango huo utakapowasilishwa, basi Kamisheni ya Ulaya, Benki Kuu ya Umoja wa Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa lazima zitathmini ikiwa hali ya sarafu ya Euro inalazimisha kuisaidia Ugiriki."
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.amesema, kuna masharti ya kutimizwa. Kwanza, mpango unaoaminika kupunguza matumizi, ujadiliwe kati ya Ugiriki, Kamisheni ya Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa. Pili, mpango huo utakapowasilishwa, basi Kamisheni ya Ulaya, Benki Kuu ya Umoja wa Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa lazima zitathmini ikiwa hali ya sarafu ya Euro inalazimisha kuisaidia Ugiriki."Baada ya kutimizwa kwa masharti hayo mawili, masuala mengine kuhusu kiwango na njia ya kutoa msaada huo yanaweza kujadiliwa.
Rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad, amewasili nchini Uganda, ambako suala la mpango wa nuclear la Teheran linatarajiwa kuwa agenda kubwa katika mazungumzo yake na Rais Museveni.
Kwa hivi sasa Uganda ni mwanachama katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Siku ya Ijumaa, katika siku yake ya pili ya ziara nchini Zimbabwe, Bw Ahmadinejad aliyashtumu mataifa ya magharibi kwa kujaribu kuangamiza uchumi wa Iran na Zimbabwe.
Akifungua maonyesho ya biashara mjini Bulawayo, Bw Ahmadinejad alisema nchi hizo mbili zilipitia wakati mgumu wa kuingiliwa kati na mataifa hayo ya magharibi.
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ameunga mkono mpango wa nuclear wa Iran.

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ameunga mkono 'kusudio halali' la Iran kutengeneza nishati ya nyuklia.
Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad anamalizia na ziara yake nchini Zimbabwe. Rais huyo baadaye ataelekea Uganda.
Kiongozi huyo wa Zimbabwe amesema nchi yake pamoja na Iran 'zimekashifiwa na kuadhibiwa visivyo halali na nchi za Magharibi'.
Iran inakabiliwa na vikwazo vya kibiashara na kidiplomasia kutoka Umoja wa Mataifa, ingawa nchi hiyo imesisitiza kuwa miradi yake ya nyuklia sio ya kutengeneza silaha.
Bw Ahmadinejad anatazamiwa kufungua maonesho ya biashara mjini Bulawayo.
Hata hivyo chama cha waziri mkuu Morgan Tsvangirai,MDC, kimelaani ziara hiyo, na hakikutuma mwakilishi yeyote kwenda kumpokea rais wa Iran alipowasili.
Chama hicho kimesema kumualika rais huyo kufungua maonesho ya biashara, ni sawa na 'kualika mbu kutibu malaria'

UTAFITI umeonyesha kuwa zaidi ya nusu ya mawaziri waliotajwa kuwa makamanda katika Serikali ya Awamu ya Nne wanaweza kupoteza nafasi zao za ubunge kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2010.
Kwa mujibu wa asasi isiyo ya kiserikali, Nyota, iliyofanya utafiti huo katika kipindi cha miezi sita iliyopita, hali ni tete katika majimbo ya mawaziri hao.
Mawaziri hao wako hatarini kukosa ubunge kutokana na wananchi wengi wa majimbo hayo kukosa imani nao, baada ya kaulimbinu ya ‘maisha bora kwa kila Mtanzania’ kushindwa kuonekana kwa vitendo majimboni mwao.
Taarifa ya awali iliyotolewa na Mratibu wa asasi hiyo, Vincent Kornald Mkisi, ilisema kuwa mazingira ya mawaziri na manaibu hao kupoteza nafasi zao yalianza kuonekana tangu Januari mwaka huu.
Mkisi alitaja majina ya mawaziri walio katika hali mbaya kurudi bungeni kuwa ni pamoja na Profesa Peter Msolla ambaye anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kilolo, Venance Mwamoto ‘Motto’.
Duru za kisiasa zinasema kuwa Profesa Msolla alitarajia kudra za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuligawa Jimbo la Kilolo na kuwa mawili, hivyo alijipanga kuwania ubunge katika eneo la Ilula ambako anakubalika zaidi kuliko maeneo mengine.
Profesa Msolla baada ya kubaini kwamba yuko katika hali mbaya kisiasa, aliamua kumtumia Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Dk. Athuman Mfutakamba, kumfanyia kampeni za wazi katika maeneo ya vijijini na wakati mwingine ‘kudandia’ ziara za mkuu huyo wa wilaya ili kuweza kuwafikia wapiga kura wengi.
Tanzania Daima Jumatano iliwahi kunasa barua ya waziri huyo kwenda kwa Mfutakamba, akimtaka amwandalie mikutano ya hadhara ya kichama huku akijua fika kwamba kiongozi huyo ni wa serikali.
Waziri mwingine anayetajwa kuwa katika kaa la moto kwa mujibu wa utafiti huo, ni Profesa Jumanne Maghembe, anayekabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mwanasheria wa kujitegemea, Joseph Tadayo.
Inaelezwa kuwa baada ya Tadayo kuweka bayana nia ya kuwania ubunge katika Jimbo la Mwanga, waziri huyo alianza mkakati wa kutumia nguvu kulazimisha kukutana na wazee kwa nia ya kuwaweka sawa na kujihakikishia kuilinda nafasi yake ya ubunge.
Hata hivyo, Profesa Maghembe anapaswa kujilaumu mwenyewe kutokana na kile ambacho wananchi wa Mwanga wamekuwa wakikitaja kuwa ni ubabe na kujiona ana haki ya kifalme ya kuliwakilisha jimbo hilo.
Lakini pia watafiti wanasema ameshindwa kuwaunganisha wananchi wa Mwanga, na kwamba hata waziri mkuu mstaafu ambaye pia alikuwa mbunge wa jimbo hilo, Cleopa David Msuya, hakubaliani naye.
Nyota imeonyesha kuwa pamoja na kuwa sura za vijana katika Baraza la Mawaziri ilionekana kuwa nuru mpya kwa wananchi na kuwafanya kuwa na imani na Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, mawaziri wake wawili vijana, William Ngeleja wa Nishati na Madini na Dk. Lawrence Masha wa Mambo ya Ndani wako juu ya kaa la moto.
Ngeleja anakabiliwa na mchumi mwandamizi na mwanamageuzi wa kilimo anayeendana na falsafa mpya ya ‘Kilimo Kwanza’, Francisco Kimasa Shejamabu, ambaye pia ni meneja na mmiliki mwandamizi wa Kampuni ya Tanwat ya jijini Mwanza.
Aidha, habari zinasema kuwa Masha, anayeongoza Jimbo la Nyamagana, anakabiliwa upinzani mkali kutoka kwa kijana mmoja msomi kutoka kwenye moja ya vyuo vikuu nchini na ambaye ameonyesha nia ya kukabiliana naye ndani ya CCM.
Kana kwamba mchakato ndani ya CCM hautoshi, Masha na Ngeleja pia wanakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa wagombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wanaokubalika katika majimbo hayo kuliko ilivyo kwa mawaziri hao.
Habari zinasema kuwa Ngeleja alikuwa akiandaa mkakati wa kutaka matawi na kata za CCM katika Jimbo la Sengerema kutoa tamko la kumtangaza kuwa mgombee pekee ili aweze kupitishwa bila kupingwa.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa mpango wake huo umekwama kutokana na kuwapo kwa kundi kubwa la wanachama wa CCM walioamua kupingana na dhana hiyo na kutaka kuwapo demokrasia ndani ya chama chao.
Mwingine anayekabiliwa na hali mbaya ni Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Kapteni George Huruma Mkuchika (Newala), Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Diodoros Kamara (Nkenge), Waziri wa Sheria na Katiba, Mathiasi Chikawe (Nachingwea), Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo (Kilosa Kati), Waziri wa Kilimo na Chakula, Stephen Wassira (Bunda) na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Mary Nagu (Hanang).
Kulingana na utafiiti huo wa Nyota, Mkisi alisema wanaamini kuwa baadhi ya mawaziri hao huenda wakaondoa majina yao kwenye mchakato ndani ya CCM kwa hofu ya kupata aibu.
Mbali na mawaziri hao waandamizi, utafiti huo pia umewataja manaibu waziri walio katika hali mbaya majimboni mwao.
Mawaziri hao ni pamoja na Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Emmanuel Nchimbi (Songea Mjini), Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana, Dk. Milton Makongoro (Ukonga). Hata hivyo, Dk. Mahanga anaweza kupumua baada ya NEC kuligawa jimbo hilo katika majimbo mawili.
Wengine ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Kighoma Malima (Mkuranga), Naibu Waziri wa Uvuvi na Ufugaji, Dk. James Wanyancha, (Serengeti), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Seif Ally Idd na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami (Moshi Vijijini).

• YAKIRI KIUTU UZIMA KUCHOMEKA VIPENGELE KINYEMELA
HATIMAYE Mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa (CHADEMA) ameibwaga serikali.
Ingawa ilikuwa imekana madai aliyotoa kuwa imechomeka kinyemela vipengele kwenye Muswada wa Sheria za Gharama za Uchaguzi uliosaniwa kwa mbwembwe kuwa sheria na Rais Jakaya Kikwete mwezi uliopita, juzi jioni iliurudisha bungeni ili kufanya marekebisho ya kuvinyofoa vipengele hivyo.
Muswada huo wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali wa mwaka 2010, ikiwemo Sheria ya Udhibiti wa Gharama za Uchaguzi, uliwasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema.
Werema ndiye aliyekuwa ameahidi awali, Dk. Slaa alipoibua hoja hiyo, kwamba kama serikali ingegundua kuwa vifungu hivyo vilichomekwa kinyemela, ingeomba radhi na kuurudisha muswada bungeni ufanyiwe marekebisho; ingawa baadaye alimbeza mbunge huyo, akajiingiza katika malumbano ya kutoa “ufafanuzi” wa kilichotokea, akasema vifungu viliongezwa ili kutafsiri kilichokuwa kimepitishwa na Bunge.
Lakini kitendo cha serikali kurejesha Sheria ya Gharama za Uchaguzi kwa ajili ya marekebisho bungeni, kimetafsiriwa na wachambuzi wa masuala ya siasa nchini kuwa ni ushindi wa Dk. Slaa dhidi ya serikali.
Werema aliwasilisha muswada huo unaolenga kuzifanyia marekebisho sheria 16 zilizotungwa na Bunge, ikiwemo sheria namba 6 ya mwaka 2010.
Moja ya vipengele vilivyofanyiwa marekebisho ndani ya sheria hiyo, ni pamoja na kifungu cha timu ya mgombea kuhakikiwa na msajili wa vyama vya siasa, kilichokuwa kinalalamikiwa na Dk. Slaa. Sasa kimeondolewa.
Dk. Slaa katika madai yake, alikuwa amepinga kifungu hicho kwa madai kuwa kinakwenda kinyume cha misingi ya demokrasia, kwani timu za wagombea zingeweza kuondolewa kwa utashi wa msajili au ofisa mtendaji wa kata.
Akitetea uamuzi mpya wa serikali dhidi ya kauli yake ya awali, Werema alisema: “Kilichojitokeza bungeni kama inavyoonekana katika ‘Hansard’ (kumbukumbu za Bunge) ya Februari 11, 2010 kwa nia njema na kwa kuzingatia taaluma ya uandishi, tuliona kwamba kuidhinishwa kwa wajumbe wa timu ya kampeni ilikuwa ni jambo la kuzingatiwa.
“Baada ya kupata ushauri wa kamati ya uongozi kwa ushauri wa kamati mbili zilizoujadili muswada huu, sasa dhana ya kuidhinishwa kwa timu ya kampeni naomba iondolewe na badala yake wagombea wawasilishe orodha.”
Mapendekezo hayo yanahusu pia kuondoa ulazima wa mgombea kupata ridhaa ya msajili wa vyama vya siasa au ofisa mtendaji mkuu wa kata kuhusu gharama atakazotumia katika kampeni.
“Lakini pia mabadiliko haya yanagusa siku za kuhakiki na gharama za mgombea kupunguzwa kutoka saba hadi tano,” alisema Werema.
Msimamo mpya wa Werema unaunga mkono hoja mama ya Dk. Slaa kuhusu vifungu hivyo vya sheria. Hata hivyo, serikali haijaomba radhi kama alivyokuwa ameahidi mwanasheria huyo.
“Aidha inapendekezwa kufanya marekebisho katika kifungu cha 24 (1) kwa kupunguza siku ambazo kila chama cha siasa kitatakiwa kukamilisha mchakato wa uteuzi wa wagombea ndani ya vyama kutoka siku 21 hadi tano kwa lengo la kuainisha dhana ya siku iliyopo kifungu cha 9 (1),” alisema Werema.
Mbali na sheria hiyo, sheria nyingine zinazofanyiwa marekebisho ni ile ya Benki Kuu, Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Criminal Procedure Act) na Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976.
Kwa upande wa sheria ya magazeti, mapendekezo ya muswada huo, yanalenga kuondoa ulazima wa kuwepo kwa washauri wa mahakama wakati wa kusikiliza mashauri ya kashfa za magazetini (defamation) na badala yake watakuwepo pale tu mahakama itakapoona ulazima.
Baadhi ya wabunge waliohojiwa na Tanzania Daima Jumatano, walisema kwa nyakati tofauti kuwa ndani ya mfumo wa serikali kuna kasoro nyingi.
Mbunge wa Kahama, James Lembeli (CCM), alisisitiza kuwa ndani ya mfumo wa serikali kuna kasoro nyingi, na akamtaka Rais Jakaya Kikwete kuwa makini nazo.
Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (CHADEMA), alisema hatua hiyo imeifedhehesha serikali ambayo ilikuwa imetamba, kwa kauli ya Werema, kwamba haijachomeka kipengele hicho kinyemela.
“Hii ni fedheha kubwa kwa serikali hii. Huu ni ushahidi tosha kwamba Dk. Slaa alikuwa sahihi wakati analalamikia vipengele hivi,” alisema Ndesamburo.

Rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad anatarajiwa kuwasili nchini Zimbabwe hii leo katika awamu ya kwanza ya ziara yake barani afrika.
Ahmadinejad vile vile anatarajiwa kuzuru Uganda wakati wa ziara yake barani Afrika. Mbali na kujadili masuala ya kibiashara na kiuchumi, rais huyo wa Iran anatarajiwa kujadili mpango wa nchi yake wa Nuklia na rais wa Uganda Yoweri Museveni.
Mwaka uliopita utawala wa Teheran ulikataa mpango ulioungwa mkono na Umoja wa Mataifa, ambapo Iran ingepokea mafuta itakayotumika kwenye viwanda vyake vya nuklia ikiwa itasalimisha akiba yake ya madini yaliyorotubishwa ya Uranium.
Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Manouchehr Mottaki, amesema ujumbe wa Iran, utapendekeza mpango mbadala wa mafuta ya viwanda vyake vya nuklia, wakati wa ziara yao katika nchini wanachama wa kudumu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa.
Uganda na Lebanon, ni wanachama wa baraza hilo la usalama la umoja wa mataifa.

BAO lililofungwa na Steve Bengo wa Yanga katika dakika ya 87, lilitosha kuishusha Prisons ya Mbeya Daraja la Kwanza, baada ya miaka 15 katika mchezo wa kufunga pazia wa Ligi Kuu uliofayika kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Prisons iliyotoka sare ya 1-1 na Yanga, sasa inaungana na Moro United na Manyema kushuka daraja na sasa zitacheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao.
Nafasi za timu hizo zimeshazibwa na AFC Arusha, Polisi Dodoma na Ruvu Shooting zilizopanda Ligi Kuu msimu ujao baada ya kushika nafasi tatu za juu, michuano iliyofanyika mkoani Arusha.
Prisons ilikuwa iokoke kama ingeifunga Yanga, lakini dakika tatu, zilitosha kuimaliza timu hiyo baada ya kuongoza kwa bao la Sospeter Wenga aliyefunga bao dakika ya 70 ikiwa ni dakika 10 baada ya mchezaji wa Prisons, Fred Chudu kutolewa kwa kadi nyekundu.
Kwa upande wa Manyema iliyotoka suluhu jana, ilikuwa ikihitaji ushindi tu dhidi ya Azam iweze kukwepa kushuka, kwani ingefikisha pointi 25 ambazo ni zaidi ya Majimaji na Kagera zilizomaliza zikiwa na pointi 24.
Ukiacha timu hizo zilizoshuka, Simba imeweka rekodi ya aina yake msimu huu baada ya kumaliza ligi kwa kishindo kwa kuizabua Mtibwa Sugar ya Morogoro mabao 4-0 katika mchezo mkali uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Simba imetwaa ubingwa mwaka huu kwa kufikisha pointi 62 ikiwa haijapoteza hata mchezo mmoja huku ikiwa imefunga mabao 50 na kufikisha pointi 62. Yanga ni ya pili baada ya kufikisha pointi 49.
Mshambuliaji wa Simba Mussa Hassan Mgosi ameibuka mfungaji bora kwa kupachika mabao 18 sawa na mfungaji bora wa msimu uliopita, Boniface Ambani.
Timu zilizosalimika ni Azam FC na African Lyon ya Dar es Salaam, Mtibwa Sugar ya Morogoro, JKT Ruvu ya Pwani, Toto African ya Mwanza, Majimaji ya Songea na Kagera Sugar ya Kagera.

BUNGE la Muungano limedhiria kwa pamoja Azimio la Itifaki ya Pamoja la Soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki huku kukiwa na shaka kubwa katika itifaki hiyo.
Azimio hilo lilipitishwa kwa msaada mkubwa wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda pamoja na Spika wa Bunge, Samuel Sitta ambao muda wote walikuwa wakiwasihi wabunge wasikumbuke vidonda ilivyopata Tanzania katika mkutano wa Doha .
Pamoja na ushawishi mkubwa kutoka kwa viongozi hao, lakini mbunge wa Kahama, James Lembeli alionyesha wasiwasi wake na kutamka kuwa anaunga mkono kwa shingo upande hali iliyoonyesha kuwa hakuridhika lakini haikuwa busara kupingana na Waziri Mkuu.
“Mbele ya safari ni kiza kinene kwani ndoa hii ina shaka sana inaweza kuvunjika muda na wakati wowote kwani inaniuma sana kuona serikali iko kimya hata baada ya mkutano wa Doha imeshindwa kukemea tatizo hilo, ” alisema Lembeleli
Mbunge huyo alisema yako meno ya tembo ambayo yanaigharimu serikali kiasi cha Sh 200 milioni kwa ajili ya kuyatunza kwa kila mwaka, lakini walipotaka kuyauza Wakenya walisingizia kuwa yakiuzwa pesa zake zitatumika kufanyia kampeni za uchaguzi.
Mashaka ya wabunge hao yalielekezwa moja kwa moja katika nchi ya Kenya ambayo walisema imekuwa haionyeshi ushirikiano wa dhati na majirani na kwamba inaoyesha kuwa na tamaa kwa vitu ambavyo vinatoka Tanzania .
Msuguano wa wabunge ulianzia katika semina iliyoitishwa na jumuiya hiyo ambapo Wabunge walichachamaa na kumtaka rais kukataa kupitisha azimio hilo licha ya kuwa rais alishasaini mkataba wa ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe aliwataka wabunge wakubaliane kwa pamoja kupitisha azimio hilo kwa madai kuwa kama Watanzania wataogopa watakuwa wanaonyesha woga kuingia katika soko hilo la ushindani.
Kabwe aliwataka wabunge wawe makini katika kujadili jambo hilo kwa masilahi ya wananchi wao na akatahadharisha kuwa wanasiasa na wafanyabiashara wa Kitanzania wote wamekuwa wakiongea lugha ya woga kwa kuwaogopa Wakenya tu.
Kwa upande wake Rymond Mrope alisema kuwa kitendo kiichofanywa na Wakenya katika mkutano wa Doha hakivumiki na akasema ujirani wao siku zote ni ujirani wa mashaka.
“Ujirani wetu na Wakenya siku zote ni ujirani wa mashaka na hapa tunasema kuwa tukijibu mapigo hawa jamaa wataumia sana lazima wafahamu kuwa ujirani wowote ni kufaana waambieni” alisema Mrope.
Mbunge wa Same Mashariki Anne Kilango Malecela yeye alitahadharisha serikali kuhusu azimio hilo ambapo alisema tayari Wakenya walishaanza mapema kuingia katika soko hilo kwani alisema kabla ya kuridhiwa lakini vijana wengi wa nchi hiyo wanafanya kazi Tanzania .
“Kabla hata ya kipenga kulia lakini Wakenya walishaanza kucheza mpira hii ni aibu kubwa sana tena wanawafedhehesha wananchi wetu kwa kusema eti hawajui kuongea Kingereza bila ya kujua kuwa sisi tunazungumza Oxford yenyewe kuliko hata wao, nasema watimuliwe kwanza ili tuanze utaratibu mpya” alisema Kilango.
Mbunge huyo pamoja na Dk Binilith Mahenge waliitaka serikali kuachana kabisa la suala la ardhi kuingia katika mfumo huo kwa madai kuwa nchi tano zinazoingia katika soko hilo ni Tanzania peke yenye ardhi.
Katika mchango wake mbungewa kuteuliwa na rais Ismail Jusa Radu alionyesha wasiwasi katika Azimio hilo kwani alisema hauonyesha wazi sehemu ya Zanzibar katika soko hilo itakuwa wapi.
Akitoa majumuisho ya michango ya wabunge Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk Diodorus Kamala aliwata wabunge kutokuwa na mashaka juu ya Azimio hilo kwa kusema kuwa Tanzania itakuwa makini katika masuala yote yanayohusu masilahi ya nchi.
Kuhusu suala la ardhi Kamala alisema kuwa hilo halitawezekana kutokana na ukweli nchi nyingi za jumuiya hiyo hazina ardhi hivyo zinaweza kuchukua ardhi ya Watanzania kama viongozi hawatakuwa makini.

LICHA ya kutangaza kutogombea urais mwaka 2010, waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye bado anatajwa katika anga za kisiasa baada ya kuelezewa kuwa ni mmoja wa watu wanaoweza kujitokeza kupambana na Jakaya Kikwete katika kinyang'anyiro cha urais.
Sumaye, ambaye alikuwa waziri mkuu kwa kipindi cha miaka kumi, alijitokeza kuwania kuteuliwa na CCM kuwania nafasi hiyo mwaka 2005, lakini hakuweza kufua dafu.
Baada ya kumalizika kwa uchaguzi, alikwenda masomoni nchini Marekani na aliporejea aliweka bayana kwamba elimu yake ya juu zaidi aliyokwenda kuipata haikuwa na uhusiano na urais wa 2010 na mara kwa mara amekuwa akisisitiza kutokuwa na mpango wa kugombea kiti hicho mwaka huu.
Alisema hata utaratibu wa CCM wa kumuachia mshindi wa kiti cha urais kuachiwa aendelee ngwe ya pili, unamzuia kujitokeza kuwania urais.
Lakini, taarifa za kuaminika kutoka vyanzo mbalimbali zinasema Sumaye ni mmoja wa watu wanaoweza kubadili hali ya kisiasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi wa Oktoba mwaka huuu.
Alipoulizwa jana kwa njia ya simu, alisema: "Nimetoa msimamo wangu mara kwa mara kuhusu jambo hili (la urais), kwa hiyo kama kuna watu wananitaja na kuniona nafaa, mimi nasema bado sijawaona wala kuwasikia."
Sumaye, ambaye alizungumza katika hali inayoashiria kuwa ni mwenye furaha, aliongeza: "Kama wakitokea watu wakiniambia nigombee urais, nitawauliza kwa nini wanataka mimi nigombee; wanafikiri nina kitu gani ambacho naweza kukifanya?"
Alipoulizwa kama kutatokea watu na kumtaka abadili msimamo wake ili aweze kugombea urais, alicheka kisha akajibu: "Aaaa... sasa tatizo hao watu hawajajitokeza na kuniambia hivyo, wangekuwa wapo tayari ningeweza kuwapa jibu baada ya kuwauliza.
"Pia ningeweza kuwa na jibu kwako, lakini siwezi kujibu kitu kwa jambo ambalo sijalipata rasmi wala sijui ni nani anazungumza hivyo, ila wakiniambia siku nitawapa jibu."
Huku akiendelea kucheka Sumaye alihoji : "Au wewe (mwandishi) ndiyo unataka mimi Sumaye nigombee urais? Ninachoweza kusema hadi sasa sijamsikia mtu akitaka nigombee urais. Ila wewe kama ndiyo unasema Sumaye nigombee urais sawa ni maoni yako."
Sumaye alisema anafahamu kuwa hadhi yake ni mali ya umma na umma unaweza kumwomba afanye kitu fulani, lakini bado alisisitiza: "Sijawasikia hao watu wanaonitaja mimi nigombee urais."
Sumaye alisema hadi sasa bado yuko CCM na kwamba kama kuna mipango yoyote ni ile inayofuata taratibu za chama. Waziri mkuu huyo mstaafu alisema kwamba umma ni sehemu kubwa na kwamba hadi sasa hajaelewa genge hasa ambalo linamtaka yeye kugombea nafasi hiyo na mantiki inayokusudiwa.
Vyanzo vyetu vimebainisha kuwa uamuzi wa kumtaka agombee kiti hicho ni ombi maalumu kutoka kundi maalumu la watu wa kada mbalimbali nchini. Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, tayari kundi hilo limejipanga vema ikiwa ni pamoja na kufanya hadi utafiti kuhusu asilimia za kura za urais ambazo Sumaye anaweza kuzipata kama ataingia katika kinyang'anyiro hicho kwa kumvaa Rais Kikwete.
Ingawa tafiti mbalimbali ikiwemo za Synovate zinamuonyesha Rais Kikwete kuweza kupata asilimia zaidi ya asilimia 50 katika uchaguzi ujao, vyanzo hivyo vinaonyesha kama Sumaye ataingia anaweza kupata asilimia 40 ya kura za urais huku Kikwete akipata asilimia 52.
Vyanzo hivyo vya habari vilifafanua kwamba Sumaye amekuwa akiandaliwa mipango mbalimbali ambayo kwa sasa imefikia katika hatua ya juu ya kiutekelezaji kumwezesha kutimiza azma hiyo ya kumvaa Kikwete.
Katika taarifa hizo, vyanzo hivyo vinasema Sumaye anaonekana kuwa mtu makini na mwenye maono na ana uzoefu unaoweza kuleta changamoto kubwa za maendeleo kutokana na kukaa madarakani akiwa ni waziri mkuu kwa kipindi kirefu cha miaka 10.
Siku za karibuni Sumaye amekuwa akijitokeza hadharani katika matukio mbalimbali na hata mwishoni mwa mwaka jana alishiriki kikamilifu katika kongamano la hali ya kisiasa nchini lililoandaliwa na Taasisi ya Mfuko wa Mwalimu Nyerere na kufanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Katika kongamano hilo Sumaye alikuwa akitaka kusomwa kwa maazimio yaliyotolewa na wananchi bila kuchelewesha, lakini mwenyekiti wa kongamano, Dk Salim Ahmed Salim alishauri ufanyike uhariri kidogo kutokana na maazimio hayo kuwa makali zaidi kwa serikali ya Rais Kikwete.
Kongamano hilo hadi sasa limebaki kuwa tukio kubwa ambalo serikali na CCM iliwaelezea waliohudhuria kwamba ni watu ambao walikuwa na chuki kutokana na kukosa madaraka baada ya uchaguzi wa chama wa mwaka 2005.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa Mwananchi, kundi hilo la watu mashuhuri wakiwamo viongozi wa dini, wanasheria, wanaharakati na viongozi wa vyama vya upinzani wamekwishaweka mkakati maalum wa kumshauri Sumaye kugombea urais kupitia chama kimojawapo cha upinzani.
Hatua hiyo ya kumshauri Sumaye kugombea inaweza kusababisha mpasuko mkubwa ndani ya CCM na hata wale ambao watatoswa kwenye kura za maoni. Hata hivyo, CCM kwa kujua hilo imeweka tarehe ya kuteuliwa kwa wagombea siku mbili kabla ya siku ya mwisho kwa Tume ya Uchaguzi kupokea majina rasmi.

Zimbabwe inaadhimisha miaka 30 ya uhuru wake kutoka wa Uingereza.
Sherehe za maadhimisho hayo ni pamoja na kuimba nyimbo na kucheza muziki usiku kucha katika mji mkuu wa Harare, na kufuatiwa na hotuba kutoka kwa rais Robert Mugabe.
Bw Mugabe, ambaye ametawala tangu mwaka 1980, anaongoza serikali ya muungano kwa kushirikiana na mpinzani wake Morgan Tsvangirai, ambaye ni waziri mkuu.
Katika maadhimisho haya, kundi moja la haki za kiraia limesema wajumbe wake wanne wamenyimwa dhamana, baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kufanya maandamano kinyume cha sheria.
Kundi hilo limekanusha kufanya makosa yoyote.
Wajumbe wanne wa kundi hilo la wanawake, walikuwa sehemu ya kundi la wanawake waliokuwa wakiandamana kupinga ukataji umeme na bei kubwa ya nishati hiyo nchini Zimbabwe

MAWAZIRI wawili jana waliungana na wadau mbalimbali wa sekta ya madini, wakiwemo wachimbaji wadogo, kupinga muswada wa sheria mpya ya madini na hivyo kumuweka kiti moto Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.
Tofauti na utamaduni wa siku zote wa uwajibikaji wa pamoja, Stephen Wassira, ambaye ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, na Ezekiel Maige, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, waliungana na wengine kukosoa muswada huo wakisema umejaa mapungufu makubwa na unalenga kunufaisha wachimbaji wakubwa na kuacha wadogo.
Mwanasheria mkuu wa zamani wa serikali, Andrew Chenge ambaye ni mbunge wa Bariadi Magharibi, pia alikuwa ni mmoja wa watu walioshiriki mkutano wa siku moja baina ya wadau wa madini na wabunge, akitaka muswada huo ujadiliwe upya kabla ya kuwasilishwa bungeni.
Muswada huo ulitakiwa ujadiliwe leo na kupitishwa baada ya habari kueleza kuwa Rais Jakaya Kikwete alitoa hati ya dharura ya kuharakishwa kwa taratibu za kuupitisha, lakini hata kabla ya kuingia bungeni mambo yanaonekana kuwa magumu na huenda ratiba ikabadilishwa ili ujadiliwe baadaye.
Tayari Bunge limeshakataa miswada miwili iliyowasilishwa na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na ule ulirejeshwa mwaka jana wa Sheria ya Baraza la Usalama wa Taifa uliowasilishwa na Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), huku Sheria ya Gharama za Uchaguzi iliyopitishwa mapema mwaka huu ikitarajiwa kujadiliwa upya na mkutano huu.
Dalili za mkutano huo wa wadau wa madini na wabunge kuonekana kuwa mbaya kwa Ngeleja zilianza kujitokeza wakati Waziri Maige alipokuwa wa kwanza kuchangia aliposema kuwa muswada huo unaonekana wazi kumnufaisha zaidi mchimbaji mkubwa na kumuacha mdogo.
Sehemu mojawapo ya muswada inaeleza mchimbaji mdogo haruhisiwi kupata leseni ya kufanya utafiti, zaidi ya leseni ya kuendesha uchimbaji tu huku mchimbaji mkubwa akipewa miaka mitano kufanya utafiti kabla ya kuanza rasmi kuchimba madini.
Katika maana nyingine, alisema, mchimbaji mdogo atapaswa kulipa kodi mara tu anapoanza kazi ya kuchimba madini wakati mkubwa anaachwa kuendesha shughuli za madini kwa miaka mitano bila ya kulipa kodi, kitu ambacho wadau wa madini, walisema hakifai.
"Muswada huu haufai kwa sababu hauna sehemu yoyote inayoonyesha kuwa itamsaidia mchimbaji mdogo. Kibaya zaidi waziri amejipa madaraka makubwa ya kuamua moja kwa moja mambo mengi dhidi ya madini, kitu ambacho si sahihi," alisema Amani Mnginda wa asasi inayofuatatilia masuala ya sera, Policy Forum.
Kauli ya Mnginda iliungwa mkono na Waziri Wassira ambaye alishauri sheria ilenge kuangalia nani anapata nini.
Wassira alitoa mfano kwamba wakati fulani alikuwa kwenye mkutano wa uchumi nchini Uswisi ambako alikutana na waziri wa madini wa Sweden na kumuuliza wanafanya nini ili kuhakikisha nchi inanufaika.
"Alinijibu kwa kifupi kwamba kipaumbele chao ni wawekezaji wa ndani," alisema Wassira.
"Wazungu ambao ndio wenye kumiliki biashara ya madini siwaoni… namuona hapa (mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Madini, Amin) Mpungwe …aaah huyu ni mwenzangu mimi tu, kuna wenyewe, wako wapi?
"Ninachotaka kusema ni kwamba, tuangalie namna ya kunufaika na madini yetu. Hata wenzetu wa Afrika Kusini wana maendeleo; wamejenga barabara za juu kwa juu kwa sababu wametumia vizuri madini yao. Kama hatutakuwa makini Watanzania tutabakia na mashimo tu.
Wassira alisema inasikitisha kwamba baadhi wa wawekezaji wa kigeni wamekuwa wakinunua mbogamboga na hata maji ya kunywa kutoka Ulaya, hivyo kuwakosesha mapato Watanzania ambao wangeweza kuuza mazao yao kwao.
Katibu wa Chama cha Wachimbaji Madini wa Wilaya ya Ulanga, Christoms Msakamba alisema muswada huo unapaswa kujadiliwa na wadau kabla ya kuwasilishwa bungeni, akisema una kasoro nyingi.
"Baadhi ya kasoro hizo ni mfumo wa utoaji leseni ambao kimsingi unaonyesha kuendelea kumnyonya mchimbaji mdogo hasa kwa kutompatia unafuu wowote, huku mchimbaji mkubwa akipatiwa nafasi ya kuendesha tafiti kwa zaidi ya miaka mitano bila kutakiwa kulipa kodi," alisema.
Msakamba pia alilalamikia muswada kupendekeza nafasi ya naibu kamishna wa madini iondolewe, na kuongeza kwamba hiyo itachangia usumbufu kwa wadau wa madai hasa katika utoaji wa leseni.
"Sasa hivi pekee kuna maombi zaidi ya 5,000 ya leseni hayajafanyiwa kazi pale wizarani. Tukisema tuondoe nafasi ya kamishna msaidizi, maana yake ni kuongeza hali mbaya ya utendaji," alisisitiza.
Waziri Ngeleja alisema kuwa wizara yake itafanyia kazi maoni hayo.
Kwa sasa Sheria ya Madini inayotumika nchini ni ya mwaka 1998 ambayo imekuwa ikilalamikiwa kuwa inanufaisha zaidi wageni hasa katika suala la mrabaha wa asilimia tatu kwa wakia.
Alipoingia madarakani Rais Jakaya Kikwete aliahidi kupitia upya sheria ya madini na kuifanyia marekebisho na tayari hadi sasa mikataba ya madini ilikwishapitiwa na Tume ya Jaji Mark Bomani na kupendekeza hatua za kuchukua.
Miongoni mwa hatua hizo ni pamoja na kuhakikisha asilimia 60 ya fedha za mauzo ya dhahabu zinawekezwa kwenye mabenki ya nchini ili kuongeza thamani ya shilingi na kukuza uchumi wa nchi.

HALI ya kisiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imezidi kuwa tete, baada Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuitisha kikao cha dharura cha wabunge wa chama hicho mjini Dodoma juzi kwa ajili ya kujadili na kukemea tabia ya kupakana matope wakati huu wa kuelekea katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba.
Habari za kuaminika ambazo Tanzania Daima Jumapili limezipata kutoka ndani ya kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa zamani wa Bunge wa Pius Msekwa, zinasema kikao hicho kilitawaliwa na mjadala mkali wa baadhi ya wana CCM, hasa waliotangaza nia ya kugombea ubunge katika majimbo mbalimbali.
“Ni kweli tulikutana wote chini ya Mwenyekiti wetu, Waziri Mkuu jana (Ijumaa) kujadiliana masuala mbalimbali, lakini moja ya ajenda kubwa iliyoonekana ni suala zima la mwenendo unaonyesha namna baadhi ya watu waliotangaza nia ya kugombea ubunge wanavyowapaka wabunge walioko madarakani matope.
“Wabunge wengi wamepinga utaratibu ambao umeanza kutumika kuruhusu watu kupita kwenye majimbo na kuanza kunadi sera zao kabla ya tarehe ya kampeni kufika, hawa wameonekana wazi kabisa wameanza kupiga kampeni hadharani.
Chanzo hicho kilisema watu hao wameanza kupita maeneo mbalimbali ikiwemo misikitini, makanisa na kwenye mikusanyiko ya watu huku wakitoa misaada mbalimbali kama fedha, nguo, vifaa vya michezo na ahadi mbalimbali ambazo kwa namna moja au nyingine zinakuwa na lengo la kujipigia debe.
Kiliongeza kuwa malalamiko hayo yalimfanya Waziri Mkuu kukemea vikali tabia hiyo ambayo si tu inakiaibisha chama bali inajenga uhusiano mbaya miongoni mwa wanachama ambao katika siku za hivi karibuni wamekuwa na uhusiano mbaya kiasi cha kukifanya chama kuunda kamati ya kutafuta chanzo cha kutoelewana na kuangalia namna bora ya kusuluhishana.
“Pinda ameagiza wanachama wote ambao wameanza mchezo huo wafuatiliwe, na majina yao yawasilishwe kwenye mamlaka husika ili wachukuliwe hatua za kinidhamu; lakini pia wasiteuliwe wakati wa mchakato wa kugombea ubunge,” kilisema chanzo kingine.
Tanzania Daima Jumapili ilidokezwa kuwa Waziri Mkuu ameagiza zichukuliwe hatua kwa watumishi wote wa serikali ambao wametangaza nia ya kugombea ubunge kuwa kwa kufanya hivyo wamekiuka sheria na kanuni za utumishi wa umma.
Chanzo kingine kimedokeza kuwa Waziri Pinda alisema kuna zaidi ya wakuu wa mikoa 10 na wakuu wa wilaya wapatao 30 wametangaza nia ya kugombe ubunge katika uchaguzi mkuu ujao huku wengine wakitumia nafasi zao kufanya kampeni na kuwachafua wenzao.
“Alituambia kuwa watumishi wa serikali waliotangaza nia ya kugombea ubunge wakiwemo ma-RC na ma-DC, wanapaswa kuchukua likizo ya bila malipo ili wakatumikie siasa hadi uchaguzi mkuu utakapomalizika,” kilisema chanzo hicho.
Habari zaidi zinasema kuwa ameonya viongozi hao ambao wamekuwa wakitumia posho za serikali na magari kwenda majimboni kwa ajili ya kuweka mikakati mbalimbali ya kampeni huku wakitumia fedha za walipa kodi kwa ajili ya masilahi binafsi jambo ambalo halikubaliki na ni kinyume na sheria za utumishi wa umma.
Pinda alikwenda mbali zaidi kuwa watendaji hao wapo hatarini kupoteza kazi zao kama hawatajirekebisha kwa kuwa tayari baadhi ya majina yao yameshatajwa kwenye ngazi za juu za uongozi serikalini.
Chanzo hicho kilisema, idadi kubwa ya wabunge waliohudhuria mkutano huo waliishambulia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwa imekuwa chanzo kikubwa cha kuwalinda baadhi ya vigogo wanaopita majimbo na kutoa misaada bila kuogopa kukamatwa.
“Wabunge wengi wameilalamikia TAKUKURU mno kuwa imekuwa chanzo cha kuhifadhi vigogo ambao wameanza kupita majimboni na kugawa misaada, tunaamini kwa vile wengi wao ni watumishi wa serikali inaona aibu kuwakamata,” kilisema chanzo chetu.
Kutokana na hali hiyo, maafisa wa TAKUKURU wameagizwa mara moja kusoma na kuelewa Sheria ya Gharama za Uchaguzi waielewe vyema badala ya kukurupuka na kukamata wanasiasa hovyo.
“Unajua imeonekana TAKUKURU imeanza kamatakamata kila sehemu kwenye majimbo mbalimbali… hata kwa wabunge ambao kisheria bado wako madarakani kwa mujibu wa sheria hadi Bunge litakapovunjwa… wametakiwa wakasome vizuri sheria hii.
“…Unaelewa kuwa sisi wabunge tuliahidi mambo mengi mwaka 2005, sasa unapokwenda kwa wapiga kura kutoa misaada uliyoahidi unaonekana kama unatoa rushwa jambo ambalo si cha kweli,” alisema mmoja mbunge mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Hoja nyingine iliyojadiliwa kwenye kikao hicho, ni namna ya kifungu namba 7 (c) ambacho kiko kwenye Sheria ya Gharama za Uchaguzi kinavyoelezea muundo wa timu za wagombea kuanzia ngazi ya udiwani na ubunge zinavyotakiwa kuwa chini ya viongozi wa serikali.
“Imeonekana wazi kwamba kwenye muundo wa timu za wagombea kuna kasoro za usimamizi… sasa imeshauria maafisa ya serikali kuanzia ngazi ya kata wajumuishwe kwenye timu hizo.
Mkutano huo wa CCM unafanyika huku kukiwa na wingu zito wa namna mgogoro uliozuka baina ya makundi yanayohasimiana ndani ya chama hicho ambalo limechangiwa kwa kiasi kubwa na tuhuma za ufisadi utakavyosuluhishwa na kamati iliyoundwa na Halimashauri Kuu ya CCM (NEC) chini ya uenyekiti wa Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi.
CCM inadaiwa kugawanyika katika makundi mawili ambapo moja linadaiwa kuwa katika upande wa Spika wa Bunge Samuel Sitta ambaye anasemekana kuwa mstari wa mbele kutaka vigogo wa ufisadi washughulikiwe ndani na nje ya chama huku kundi la pili linalodaiwa kuongozwa na aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa likidaiwa kupingana na lile la Sitta kwa madai kuwa ni vema sheria zikachukua mkondo wake badala ya watu kusingizia au kuelekezeana tuhuma kwa lengo la kuchafuana.
Makundi hayo mawili yalijipambanua baada kuibuka kwa kashfa ya kuzalisha umeme wa dharura kupitia kampuni ya Richmond, kashfa iliyomsababishia Lowassa na mawaziri wawili, Nazir Karamagi (Nishati na Madini) na Ibrahimu Msabaha kuachia nyadhifa zao baada ya kuguswa na kamati teule ya Bunge iliyokuwa chini ya uenyekiti wa mbunge wa Kyela Dk. Harisson Mwakyembe.

MTANDAO hatari umeibuka jijini Dar es Salaam ukijikusanyia mamilioni ya fedha kutoka kwa vigogo na wafanyabiashara maarufu baada ya kuwatengenezea mafumanizi ya kupanga na kuwapiga picha za utupu.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini miongoni mwa waliokumbwa na mkasa huo wamo mawaziri, wabunge na wakurugenzi wa mashirika mbalimbali nchini.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, mtandao huo (majina tunayo), umekuwa ukiwatumia wasichana warembo ambao baada ya kupata namba za simu ya mkononi ya mlengwa humpigia simu kupitia (mrembo), huyo ambaye hujifanya amekosea namba.
Hata hivyo, mrembo huyo anayepiga simu huongea kwa sauti ya upole na ushawishi na kuwanasa kwenye mtego huo wanaume wenye tamaa, ambapo baada ya kukubaliana hukutana na wasichana hao kwenye hoteli mbalimbali zisizo na maarufu jijini humo kwa ahadi maalum.
Uchunguzi huo unaonyesha kuwa katika hoteli hizo, wasichana hao huwashawishi wanaume waliowanasa kuchukua chumba kwa ajili ya mazungumzo.
Imebainika kuwa wakiwa chumbani, wasichana hao huwaingiza katika mtego kama vile wanataka kufanya mapenzi na wanaume hao, huku wakihakikisha mlango wa chumba haufungwi kwa funguo na ndipo kundi la watu hutokea, huvamia na kuanza kumshambulia mwanaume husika, kumpiga picha akiwa utupu na kudai kuwa anachukua wake za watu.
Hata hivyo, gazeti hili limebaini kuwa wanawake wanaotumiwa katika mchezo huo mchafu sio wake za watu kama inavyodaiwa na wavamizi bali ni wasichana wa mitaani wenye tamaa ya fedha za haraka.
Katika mazingira hayo ya fumanizi mwanaume anayefumaniwa hulazimishwa kutoa fedha kati ya Sh10milioni hadi 20milioni huku wakimtishia kuwa endapo atakataa kutoa fedha hizo picha hizo watazichapisha katika magazetini wanayoyamiliki au kumwagwa maeneo ya wazi na katika mtandao ili watu wazione.
Kutokana na hofu ya kuchafuliwa majina yao au kuharibu ndoa zao, vigogo hao wamejikuta wakitoa fedha hizo na kuomba picha alizopigwa kwa kamera za wavamizi hao wanaodaiwa kujifanya waandishi wa habari ziharibiwe, au kuchomwa moto kwa lengo la kupoteza ushahidi.
Gazeti hili limefanikiwa kupata picha kadhaa za fumanizi ambazo zinaonyesha baadhi yao vigogo hao wakiwa katika mazingira ya purukushani na wengine wakiwa utupu huku wengine wakionekana kupokea kipigo kutoka kwa kundi la wavamizi wanaofanya fumanizi hilo la kupanga ili kujipatia fedha.
Picha ambazo uchunguzi wa gazeti hili umefanikiwa kuziona ni za vigogo wa mashirika, wafanyabiashara maarufu na watu wenye majina makubwa jijini akiwemo pia profesa ambaye mke wake ni mtu maarufu katika medani za siasa nchini.
Aidha, katika picha hizo anaonekana mmoja wa wasichana (mrembo), anayedaiwa kuishi maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam akiwa katika matukio mawili tofauti kufanikisha uharamia huo wa mamilioni.
Moja ya matukio hayo linahusisha tukio lililomhusisha kigogo wa shirika moja maarufu na tukio jingine lililomnasa profesa huyo.
Hata hivyo, habari zaidi zinaonyesha kuwa baada ya mwanaume aliyefumaniwa kushindwa kutoa kiasi cha fedha anachotaka wavamizi hao hukimbiza picha hizo kwenye magazeti ya udaku.
Msemaji mkuu wa Jeshi la polisi nchini ACP Abdallah Mssika alisema kuwa jeshi hilo bado halina taarifa za matukio hayo kwa kuwa hayajaripotiwa lakini, akasema kuwa taarifa hizo zitafanyiwa kazi.
"Inawezekana hatuna taarifa kwa kuwa matukio hayo hufanyika kwa siri na hayajaripotiwa polisi, pia wahusika wanaogopa fedheha kama baadhi ya wanawake waliobakwa wanavyoogopa kuripoti polisi, lakini matukio hayo ni mabaya na tutayafuatilia na kuyafanyia kazi," alisema.
Aliongeza kuwa vitendo hivyo ni makosa ya jinai hivyo, watuhumiwa wakinaswa watashtakiwa kwa makosa ya jinai ambapo aliwashauri waliopatwa na mkasa huo kuwa wakiogopa fedheha kuripoti polisi matukio hayo waripoti kwa afisa upelelezi na taarifa zao zitafanyiwa kazi.
Alibainisha kuwa waliokumbwa na mkasa huo wawasiliane na afisa upelelezi wa polisi mahali alipo akieleza mahali tukio lilipofanyika na kuwataja au kuelezea wahusika walivyo na magari wanayotumia ili kurahisisha kunaswa kwa watuhumiwa hao.

| Mtikila sasa kusambaza waraka wake nje ya nchi | |||||||
Akizungumza nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Slaam jana, Mtikila alisema waraka huo utasambaswa kwa waumini wa dini zote wa ndani na nje ya nchi ili wausome na baadaye kutoa maoni kama kweli unachochezi. Mtikila ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), alisema anaendelea kushangazwa na hatua ya serikali kuuona waraka huo kuwa ni wakichochezi na kwamba hawezi kuvumilia kuona nchi ikichezewa. Alisema waraka huo sasa utatafsiriwa katika lugha za kimataifa na kusambazwa katika mbalimbali wananchi wa huko wajue yanayoendelea nchini. “Siwezi kuvumilia kuona nchi ikichezewa. Nimefikia uamuzi wa kuuboresha waraka huu unaosemekana kuwa ni wa kichochezi juu ya Rais Jakaya Kikwete na wengine na sasa utatafsiriwa kwa lugha mbalimbali za kimataifa ili watu wausome na kutoa maoni yao kama ni wa uchochezi au la," alisema Mtikila. Alisema ataendelea na hatua hiyo akiamini kuwa hawezi kutiwa hatiani kwa kosa la kuandika waraka huo huku akirejea kusema kwamba iwapo akiendelea kufuatiliwa nchi itakumbwa na mabadiliko makubwa ya uongozi. Hata hivyo, Mtikia alisema hata akishtakiwa haogopi mahakama kwa kuwa ameshashtakiwa mara nyingi tangu mwaka 1988 na kwamba kwa sasa ana jumla ya kesi tofauti 46 kati ya kesi hizo ni moja pekee aliyomweka gerezani. "Siogopi mahakama kwani tangu mwaka 1988 nimeshashtakiwa kesi 46 na kesi moja tu ndio iliyoniweka ndani," alisema. Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo wa DP ametangaza nia yake kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao kama mgombea binafsi. Alisema kuwa katika uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba mwaka huu amejipanga kuchukua fomu ya kugombea urais huku akimtaka Rais Jakaya Kikwete kujiandaa kukabiliana naye. “Lazima Rais Kikwete ajiandae kwa kuwa mimi haniwezi. Katika siasa mimi nina uwezo, naamini hivyo kwa kuwa nina roho ya Kristo ndani yangu,"alisema Mtikila. Juzi Mtikila pamoja na kueleza sababu za kuandika waraka huo, alieleza kuwa kukamatwa kwake kulitokana na viongozi aliowatuhumu kupata presha ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika nchini Mwezi Oktoba mwaka huu. Alisema kuwa udini ni jambo la kuogopa na kwamba hata ibara ya 26 ya katiba inasema kuwa ni lazima kuheshimu mamlaka yeyote katika nchi kutunga sheria au kufanya jambo lolote kwa ajili ya kupendelea kikundi fulani cha dini. |
* Zitto aunga mkono, kuwashawishi wabunge waukatae
Na Frederick Katulanda, Dodoma
WAKATI serikali inatarajiwa kuwasilisha muswada wa Sheria mpya ya Madini ya mwaka 2010, viongozi wa dini ya Kikristo na Kiisalamu wamejiandaa kuupinga muswada huo na kuwashawishi wabunge kuukataa.
Viongozi dini ya ambao tayari wapo mjini Dodoma ni kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (Tec) pamoja na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT).
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili viongozi hao, walisema muswada huo ni kiini macho na kwamba, hauna dhamira ya dhati kuwawezesha Watanzania kunufaika na madini ambayo wametunukiwa na Mungu.
Afisa Mawasilino na Habari wa Jumuiya ya Kikrsto Tanzania (CCT), Mchungaji John Magafu akizungumza kwa niaba ya viongozi wa dini jana, alisema muswada huo hauna maslahi kwa taifa na kwamba, unakimbizwa haraka bungeni ili upitishwe ili kuwafurahisha wawekezaji hao.
“Sisi tunapinga kupelekwa muswada huu kwa haraka namna hiyo bungeni. Haraka ya nini wakati nchi hii ni yetu sote, tunataka tupatiwe muda wa kuchambua zaidi na kushirikisha watanzania wote.
"Madini ni mali ya watanzania wote tunataka muswada huu uendelee kujadiliwa zaidi ili uborehswe na kuwa wenye manufaa kwa taifa,†alisisitiza mchungaji Magafu.
Kuhusu upungufu uliyopo katika muswada huo, Mchungaji Magafu alisema ingawa muswada huo umeongeza tozo la mrahaba kutoka ailimia 3 hadi asilimia 4 kwa dhahabu, bado hauonyeshi kuwanufaisha wananchi wa maeneo yanayotoka madini hayo.
“Sheria hii ukiiangalia juu juu unaweza kusema nzuri, lakini haina uzuri wowote kwa vile katika mabadiliko hayo kuna upendeleo.
"Kwa mfano, ongezeko la mrahaba kampuni mpya ndizo zitakazotozwa na kuziacha zilizopo," alisema Magafu na kuhoji:
"Karibu eneo kubwa la madini limeishatolewa kwa wawekezaji, hao wapya watawekeza wapi ili tupate faidaâ€.
Mbali ya viongozi wa dini, habari zaidi zimeeleza wabunge wengi wamejiandaa kuupinga muswada huo jambo ambalo lilimshitua Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja ambaye Ijumaa iliyopita alizungumza na waandishi wa habari kuutetea muswada huo.
Ngeleja alisema muswada anaokusudia kuuwasilisha bungeni wiki ijayo umezingatia mabadiliko makubwa katika maeneo ambayo yamekuwa yakilalamikiwa kwenye sera ya madini ya mwaka 1997 pamoja na sheria ya madini ya mwaka 1998.
Hata hivyo, Magafu alidai hata madini ya 'uranium' yatalayoanza kuchimbwa katika maeneo mbalimbali, tayari nayo yameshamilikiwa na kampuni zilizopo, hivyo uwezekano wa taifa kunufaina na madini hayo unabakia kuwa ndoto.
Alisema: “Eneo lingine ambalo halikuzingatiwa katika muswada huo ni namna ya kufanya tathmini ya athari za kimazingira. Katika sheria hii inaelezwa kuwa mgodi ndiyo utaajiri kampuni ya kufanya hivyo jambo ambalo viongozi wa dini tunapinga. Tunataka iwe chini ya taasisi huru ili waweze kubanwa wawekezaji hawaâ€.
Alitoa mfano akisema Mgodi wa North Mara wakati ilipotokea athari ya maji machafu, tathmini iliyofanywa na mgodi huo ilionyesha hakukuwa na athari za kimazingira hii ni inatokana aliyeifanya alikuwa wakilipwa na kampuni ya Barrick jambo ambalo lisingekuwa rahisi kujimaliza wenyewe.
Mchunaji Magafu alisema kutokana na mapungufu hayo tayari viongozi wa dini wameunda jopo la wanasheria ambao wanauchambua muswada huo kwa kina ikiwa ni pamoja na kuuandaa kwa lugha ya Kiswahili ili uweze kusomwa na watu wote.
Naye Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe akizungumia muswada huo alisema anajiandaa kuupinga vikali iwapo utaletwa ukiwa hauna mapendekezo muhimu ya kuwanufaisha wananchi.
Alisema katika kuhakikisha unakuwa na nguvu ya pamoja atawashirikisha wabunge wote wanaotoka katika maeneo ya madini, ili kuwaomba waungane kwa maslahi ya taifa kuwa kitu kimoja kuupinga muswada huo, mpaka hapo serikali itakapokubali kuacha fedha za mrahaba katika wilaya inayochimbwa madini hayo.
Alisema katika mapendekezo ya kamati ya Jaji Mark Bomani walishauri kwamba, katika kuwashirikisha wananchi wa maeneo ya madini, serikali iwarudishie asilimia 20 katika wilaya zao ili ziweze kutumika katika miradi ya maendeleo yao, lakini serikali imegoma.
“Serikali imegoma, hii inaturudisha kule kule tulikokuwa na hakuna haja ya kuwa na sheria mpya kama haya yatazingatiwa,†alieleza.
Alisema hoja ni kuwanufaisha watu na madini yao, na kufafanua kuwa mwaka 2008/2009 serikali ilikusanya mapato katika sekta ya madini kiasi cha Sh 162 bilioni ambacho ni sawa na asilimia 16 ya mauzo yote ya nje, kati yake Sh57 bilioni zilikuwa ni mrahaba.
Alisema kiasi hicho kilipaswa kurudi kwa wananchi, lakini serikali inakataa na jambo hilo halikuzingatiwa katika muswada huo.
“Tunataka sehemu ya fedha hizo za mrahaba zirudi kwa wananchi na nyingine zianzishe mfuko wa serikali kwa ajili ya kusaidia kutengeneza barabara na mambo mengineyo. Serikali imegoma, tutaupinga muswada huu bungeni.†alieleza Zitto.
Alisema kutokana na upungufu huo na mengine atasimama kidete kuhakikisha anapinga muswada huo ikiwamo kuwashirikisha wabunge wengine kutoka maeneo ya madini.
Zitto alisema kesho anajiandaa kuzungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma kuelezea kasoro zilizopo katika muswada huo.
Ngeleja alisema kuna watu wanadai eti hata kuwasilishwa kwa muswada huu bungeni kwa hati ya dharula ni makosa.
Aliongeza kuwa kumekuwa na hofu kwa wadau wa sekta ya madini kuhusiana na muswada huo, wakidhani unaweza kuwa na mambo mazito.
Ngeleja alisisitiza muswada huo umezingatia mapendezo ya wadau wapatao 132kutoka taasisi, asasi na wachimbaji wadogo wa maeneo mbalimbali.

WABUNGE wa Chama cha Mapinduzi (CCM), walikutana juzi jioni kukubaliana kuunga mkono mapendekezo ya Mbunge wa Karatu, Dk Willibrod Slaa aliyowasilisha kwenye kamati ya uongozi ya bunge kutaka bunge lipitie upya sheria ya gharama za uchaguzi na kuifanyia marekebisho kabla ya kuanza kutumika.
Vile vile, walikumbushwa mikakati mbalimbali ikiwemo wa kulinda kura zao wakati wa uchaguzi kwa kuweka mawakala waaminifu ili zisipotee kwa wapinzani.
Habari za ndani ya kikao cha Kamati ya wabunge wa CCM, ambacho huongozwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kama mwenyekiti, kilianza saa 11:50 jioni muda mfupi baada ya kumalizika kwa bunge na kumalizika saa 2:00 usiku.
Mbali na kuzungumzia mkakati huo wa kulinda kura zao pia ulielezwa na kufafanuliwa mapendekezo ambayo Dk Slaa amewasilisha na kuelezwa kuwa wanapaswa kukubaliana nayo kwa vile hayana athari katika chama chao.
"Tulipitia mkakati wa chama wa mbinu za kulinda kura katika uchaguzi mkuu ujao ili zisipotee kwa wapinzani," alieleza alieleza mmoja wa wabunge wa CCM.
Kuhusu mapendekezo ya Dk Slaa chanzo hicho kilibainisha, “Kwa kifupi tumejadili mapendekezo yote yatakayoletwa na Dk. Slaa na kukubaliana nayo. Tumekutana kuangalia iwapo yanatuathiri… ndiyo hivyo tumekubaliana nayo na sheria hiyo itajadiliwa upya bungeni."
Hata hivyo, Spika wa Bunge Samuel Sitta aliliambia Mwananchi Jumapili wiki hii kuwa, " Tumeona katika sheria hii mambo mengi yako kinadharia, kwa mfano; sheria inasema kuwe na wajumbe wa kampeni wasiozidi 20 kwa mbunge na 10 kwa diwani na wagombea hao wawe wameidhinishwa na DAS au WEO."
"Hili ni jambo jema, lakini tafsiri yake ni kwamba serikali sasa itakuwa na ruhusa ya kukubali au kukataa nani aingie kwenye kampeni hizo na nani asiingie; na kama hiyo ndiyo tafsiri, kimsingi inaleta shida." Spika Sitta alifafanua kuwa katika bunge hili, wabunge watazitazama tena kanuni za utekelezaji wa sheria hiyo na kuzifanyia marekebisho. Dk Slaa aliliambia gazeti hili kuwa amewasilisha mapendekezo hayo kutokana na kile alichodai kuwa Rais Kikwete amedanganywa na kusaini sheria hiyo kimakosa.
Alisema aliamua kuliwasilisha suala hilo kwanza kwenye kamati ya uongozi ya Bunge ili kama angepuuzwa, alifikishe suala hilo bungeni mwenyewe kwa namna anayoona inafaa. "Mapambano ndio yameanza; mimi ni mjumbe wa kamati ya uongozi ya Bunge na leo (jana) tulikuwa na kikao, nimehoji suala hilo kabla sijalifikisha bungeni kwa namna ambayo nitaona inafaa," alisema Dk Slaa.
"Bado nasisitiza kuwa Mwanasheria Mkuu amedanganya kwa kusema vifungu hivyo viko sahihi kwa kuwa Ofisi ya (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera na Uratibu wa Bunge-, Phillip) Marmo ndio iliyovifanyia marekebisho. Ofisi ya Marmo haina mamlaka ya kubadili vifungu vya sheria iliyopitishwa na Bunge. Alisisitiza kuwa kilichojadiliwa bungeni ni vikundi vya sanaa na Bunge liliagiza viingizwe vifungu vya ufafanuzi na sio mabadiliko ya vifungu.

MWANASIASA mkongwe nchini Edwin Mtei amemtabiria mabaya Rais Jakaya Kikwete kuwa atakabiliwa na upinzani mkali katika uchaguzi mkuu ujao tofauti na chama chake (CCM) kinavyodhani.
Mtei aliyasema hayo juzi mjini hapa katika mahojiano maalumu na Mwananchi Jumapili. Aliuponda mkakati wa CCM wa kukusanya fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao.
"CCM itakabiliwa na upinzani mkali wakati wa uchaguzi mkuu tofauti na viongozi wake wanavyodhani. Hata Rais, Kikwete naye atakumbana na upinzani mkali tofauti na ushindi alioupta mwaka 2005," alisema Mtei.
Alisema matumaini ya CCM na Kikwete kuwa watapata ushindi kiurahisi ni ndoto, kwani wakabiliwa na ushindani mkubwa kutokana na wananchi kuchoshwa na utendaji wa mbovu chama hicho juu ya ahadi walizotoa mwaka 2005 ambazo hazijatekelezwa.
Kuhusu hatua ya CCM kuchangisha fedha kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao, Mtei ambaye pia ni muasisi wa Chadema huo alisema wameiga kutoka Chadema, kwa sababu sera za CCM haziwezi kuvutia wananchi.
Mtei ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu alisema mkakati huo uliozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete, hauwezi kuwavutia wala kuwashawishi wananchi kuichangia CCM na kuwa haina jipya.
"Nawaonea huruma CCM, kwani hawana jipya, hawawezi kubuni kitu kipya cha kwao. Sisi tulianza kuchangia fedha kwa njia ya uwazi na wao wamefuata nyayo; kwa kweli CCM hawana jipya,"alisema Mtei
Alidai ya kuwa sera za CCM haziwezi kuwashawishi wananchi kukichangia chama hicho na kuwa serikali CCM inayojipambanua kupiga vita rushwa imeshindwa kudhibiti mafisadi wanaotajwa ndani ya chama hicho.
"Sera za CCM kamwe haziwezi kuwavutia wananchi hadi wakichangie chama hicho, serikali inadai inapiga vita ufisadi, wakati serikali hiyo hiyo imeshindwa kuwadhibiti mafisadi na wahujumu uchumi walio ndani ya chama chao,"alisiitiza Mtei.
Akizungumzia fedha za Mfuko wa Kichocheo cha Maendeleo ya Jimbo(CDCF) zinazotarajiwa kugawanywa mwishoni mwa mwezi huu, Mtei alisema fedha hizo zitaangukia kwenye matumzi ya siasa badala ya mandeleo ya majimbo kama ilivyokusudiwa.
"Huwezi kutoa pesa kipindi hiki, hizi ndizo siasa za nchi hii. Hizi pesa za mfuko wa kichocheo cha maendeleo ya jimbo ni za siasa si za maendeleo, kwani hazina jipya,"alisema Mtei bila kufafanua.
Katika hatua nyingine Mtei pia aliishambulia CCM akidai ya kuwa imeshindwa kujali maslahi ya wananchi na kuangalia maslahi ya watu wachache ambapo alisema kuwa umasikini wa Watanzania umesababishwa na chama hicho.

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, amesema kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, na serikali yake inawaogopa Rais mstaafu Benjamin Mkapa na Mbunge wa Igunga Rostam Azizi (CCM) wanaotuhumiwa kwa kuhusika kwenye ufisadi, ndiyo maana hawajachukuliwa hatua hadi leo.
Dk. Slaa alitoa tuhuma hizo wakati akizungumza na waandishi wa habari jana nje ya ukumbi wa Bunge mjini hapa.
Katika maelezo yake Dk. Slaa alisema kuwa kutokana na tamko lililotolewa juzi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa hapo inaonyesha wazi kuwa matamshi yake yanaiweka serikali pabaya; inawalinda watu wanaohusika na ufisadi mkubwa unaoliangamiza taifa hili.
“Juzi Waziri Mkuu Pinda aliliambia Bunge kuwa hana jibu, sasa sisi wabunge tuna mamlaka ya kuhoji serikali juu ya mambo mazito ya kitaifa, lakini alichojibu ni usanii mtupu,” alisema Dk. Slaa.
Slaa alisema kuwa ana ushahidi wa vielelezo vinavyoonyesha kuwa Mkapa na Rostam walikutana chini ya mwanasheria aliyemtaja kwa jina moja tu la Sanza na kupanga mikakati yote ya kuchota fedha hizo kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.
Alisema Mkapa na Rostam walikutana katika kikao cha siri na kupitisha maamuzi ya kuchota kiasi cha sh bilioni 40 katika Kampuni ya Kagoda.
Katika hilo, Slaa alisema hata Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) nayo imehoji upotevu wa fedha hizo, lakini katika hali ya ajabu mpaka sasa haijapata majibu.
Alisema kwamba mnamo Agosti 1, 2005, Rostam na Mkapa walikutana kupanga mikakati ya kuwawezesha kuchota kiasi hicho kupitia Kampuni ya Deep Green na ilipofika Agosti 4 mwaka huo huo wakati wa mchakato wa kupata mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walifanikiwa.
“Tulitoa nyaraka kuonyesha wizi mbalimbali kuomba wazifanyie uchunguzi kampuni za Kagoda, Mwananchi na Deep green kama EPA, lakini haijafanyika kutokana na ukweli ambao tunao kuwa walizichota wao kwa ajili ya uchaguzi” alieleza na kuzidi kufafanua kuwa katika wizi wa Deep Green mambo yote yalikamilika Agosti 4 wakati CCM walipokuwa kwenye harakati za mchakato wa kupata mgombea wao kwenye kura za maoni.
“…. Hili tunalo uhakika kwani nilishawahi kuwapa mpaka Bank Statement, tulitaka uchunguzi sasa tatizo linatoka wapi kipindi chote hiki?” alihoji.
Alisema serikali imekuwa na kigugumizi kikali kutoa majibu katika kampuni mbalimbali zikiwemo Mwananchi, Tangold na Kagoda hali ambayo inaibua maswali mengi juu ya serikali kuwajibika.
“Nimetaja makampuni mengi lakini mpaka leo hii hata ile Kampuni ya Meremeta ambayo wanasema ni mali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wameshindwa kuitolea maelezo… hii inashangaza.
“…hapa tatizo si Meremeta ndugu zangu, bali tatizo ni mtu aliyehusika kwani wote wapo na wamelisababishia taifa hasara karibu sh bilioni 700 au 800, hizi zote kama zingerudi leo hii tusingekuwa na shida katika maeneo mbalimbali na kuongeza kuwa wizi hauna jeshi,” alisema Dk. Slaa.
Alisema Meremeta pekee inatuhumiwa kuchota kiasi cha bilioni 155, wakati kampuni ya Tangold inadaiwa kuchota bilioni 13 huku Mwananchi ikidaiwa kuchota bilioni 5, fedha ambazo ni nyingi kuliko za EPA.
Alisema fedha hizo zingeweza kutumika katika shughuli mbalimbali zikiwemo za ujenzi wa madarasa, kusambaza huduma za maji, umeme, kujenga zanahati na kulipa madeni ya walimu.
Alisema ni wazi kuwa serikali haina dhamira ya kweli ya kupambana na ufisadi, hali ambayo inaiweka pabaya kwa vile wananchi wataihukumu kutokana na makosa yake.
Hata hivyo, Rostam amekuwa akikana kuhusika katika ufisadi huo.
Alipoulizwa jana kwa njia ya simu, alisema maneno hayo ni ya kipuuzi.
“Hayo maneno ni ya kipuuzi; mnaniuliza kila siku na nimeshayatolea ufafanuzi?
“…Watu wamechanganyikiwa; hawajui cha kufanya katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwaka huu.
“Ni mambo ya kipuuzi na siasa zisizo na maana, kwa nini kila siku wanaendeleza hayo? Hakuna kitu cha kufanya? Tafadhali naomba msiendelee, wameshindwa kisiasa siwezi kujibishana naye,” alisema Rostam

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo imetangaza kugawa majimbo saba ya sasa ya uchaguzi ambapo bunge lijalo mwakani linatarajiwa kuwa na nyongeza ya wabunge saba wa kuchaguliwa kutoka 232 waliopo hadi 239.
Wabunge hao saba wa ziada watapatikana baada ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu kulingana na tangazo hilo la NEC.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Lewis Makame, majimbo yatakayogawanywa ni Nkasi mkoani Rukwa; Tunduru (Ruvuma); Maswa (Shinyanga); Kasulu Mashariki (Kigoma); Bukombe (Shinyanga); Singida Kusini (Singida) na Ukonga (Dar es Salaam).
“Taarifa zaidi kuhusu majimbo hayo mapya yatakayoanzishwa itatolewa baada ya Tume kukutana na wadau wa majimbo husika,” ilieleza taarifa ya Jaji Makame kwa vyombo vya habari leo.
Awali, NEC ilitangaza kwamba halmashauri zilizokuwa zikitaka majimbo yao yagawanywe, zitume mapendekezo yao kwa Tume hiyo hadi Februari 28 mwaka huu, na kwamba baada ya kufanya tathimini yake ingetangaza majimbo yanayogawanywa Aprili 10, mwaka huu.
Katika mapendekezo hayo, Tume ilisema imepokea mapendekezo kutoka halmashauri 47 nchini, zikiomba majimbo yao kugawanywa. NEC haikuzitaja halmashauri hizo. Kwa mujibu wa sheria, majimbo ya uchaguzi hufikiriwa kuongezwa kila baada ya miaka 10.
NEC ilisema maombi hayo ya halmashauri 47 yalizingatia vigezo 13 ilivyovitoa kwa majimbo yenye sifa ya kugawanywa ambavyo baadhi yao ni mawasiliano, hali ya kijiografia, idadi ya watu kwa kutumia takwimu za mwaka juzi za Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), mgawanyo wa wastani wa idadi ya watu; ambacho ni kigezo kikuu katika kuamua majimbo gani yagawanywe.
Kwa mujibu wa NEC, mgawanyo wa wastani wa idadi ya watu katika majimbo ya uchaguzi yaliyopo katika maeneo ya vijijini ni 206,130 wakati majimbo ya mjini ni 237,130.
Vigezo vingine ni uwezo wa ukumbi wa Bunge na viti maalumu vya wanawake ambavyo kwa sasa ni asilimia 30. Vingine ni mazingira ya Muungano, ukubwa wa eneo la jimbo husika, mipaka ya kiutawala na kata moja kutokuwa ndani ya majimbo mawili.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Philip Marmo, alikaririwa akisema kuna maombi zaidi ya 66 kutoka wilaya mbalimbali yaliyowasilishwa serikalini yakitoa mwito wa kuongeza idadi ya majimbo, kugawa majimbo na halmashauri mbalimbali kugawanywa.
Kati ya halmashauri zilizoomba kugawanywa majimbo ni ya Mufindi, Iringa; Kilosa na Mikumi mkoani Morogoro; Mbarali, Rungwe Magharibi na Mbozi mkoani Mbeya na Ruvuma ni Mbinga.
Maombi hayo pia yalisikika kutoka mikoa mbalimbali nchini ikiwamo Singida, Arusha, Manyara, Dar es Salaam (Ukonga na Kigamboni); Dodoma katika halmashauri za Kondoa na Bahi na Kigoma.
Kuhusu ratiba ya Uchaguzi Mkuu, Jaji Makame alisema uteuzi wa wagombea utakuwa Agosti 19 na kampeni za uchaguzi zitaanza Agosti 20 hadi Oktoba 30, mwaka huu.
“Kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi, Tume itawatangazia wananchi rasmi, tarehe ya kutoa fomu za uteuzi kwa wagombea,” alieleza Jaji Makame katika taarifa yake. Zanzibar pia imetangaza kuwa uchaguzi wake utafanyika Oktoba 31, mwaka huu.

Sitta: Zitto achana na ndoto za Geita
Vijana wa jamii ya kimasai wakilima mahindi katika kijiji cha Olerien Magaiduru wilayani Ngorongoro kamawalivyokutwa na mpigapicha wetu juzi. Vijana hao wameamua kuanza kilimo kutokana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo mwaka jana yalisababisha vifo vya mamia ya mifugo yao ndipo wakaamua kuanzisha kikundi cha Waera ili wafanye kazi hiyo waweze kupata chakula. Picha Mussa Juma
SPIKA Samuel Sitta jana alimshauri Zitto Kabwe kuachana na ndoto za kuwania ubunge wa jimbo la Geita, lakini muda mfupi baadaye kiongozi huyo wa Bunge akaomba msaada wa sala kutoka kwa paroko ili aweze kushinda uchaguzi kwenye jimbo lake.
Spika alitoa ushauri huo baada ya Zitto, ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini, kuomba kuuliza swali la nyongeza kuhusu mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Geita wakati wa kipindi cha maswali na majibu jana kwenye Mkutano wa 19 wa Bunge unaoendelea mjini hapa.
Swali la msingi kuhusu mradi huo liliulizwa na mbunge wa Geita Mjini, Ernest Gakeya Mabina, ambaye alitaka kujua kama serikali inatambua kuwa mgodi wa dhahabu wa wilayani humo uko tayari kutoa kiasi cha dola 500 milioni za Kimarekani kwa ajili mradi huo.
Baada ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), Aggrey Mwanri kujibu kuwa serikali haina taarifa hizo, Zitto, ambaye ameeleza kuwa huenda atalitosa jimbo lake na kugombea ubunge wa Geita, alisimama na kuelezea matatizo ya maji yanavyoisumbua Geita na kuiomba serikali kuangalia uwezekano wa kutoa fedha za kusambaza maji kutoka kwenye matanki.
"Kwa kuwa mgodi utatoa fedha za kukutoa maji kutoka Ziwa Victoria hadi kwenye matanki, ni vizuri serikali ikatafuta fedha ili ifanye kazi ya kusambaza maji kwenda sehemu mbalimbali," alishauri Zitto.
Lakini kabla ya kumkaribisha Mwanri kutoa maelezo, Spika Sitta alisema: "Kwanza naibu waziri ningependa kumshauri kidogo Zitto. Naomba uachane na mambo hayo ya kugombea ubunge wa Geita. Ni vizuri ukarudi kwenye jimbo lako."
Kauli hiyo ya Spika Sitta iliamsha kicheko kutoka kwa wabunge wengine.
Akizungumzia kitendo chake cha kuzungumzia masuala ya Geita mara baada ya kumalizika awamu ya asubuhi ya Bunge, Zitto alisema suala hilo halina uhusiano na uamuzi wake wa kutaka kugombea ubunge wa Geita na kwamba amekuwa akiamini ni mbunge wa watu wote na kutoa mfano jinsi alivyokuwa mstari wa mbele katika sakata la mgodi wa Buzwagi.
“Nimekuwa nikitetea Watanzania wote bila ya kujali mipaka ya majimbo, mfano ni wakati nazungumzia suala la Buzwagi. Mimi sikuwa mbunge wa Kahama, lakini nililizungumzia,†alieleza mbunge huyo kutoka Chadema.
Hadi sasa, Zitto bado hajaamua agombee wapi kati ya Kigoma Kaskazini na Geita baada ya kufanya uchunguzi ambao alisema ungetoa picha ya nini afanye kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Uchunguzi wake, ambao alisema ulifanywa na watu wake, ulihusisha majimbo ya Kinondoni, Kahama, Geita, Kigoma Mjini na jimbo lake Kigoma Kaskazini lakini baadaye akasema kuwa ameachana na majimbo matatu na kubakiwa na Geita na Kigoma Kaskazini na kwamba angetangaza uamuzi wakati wowote.
Baada ya kipindi cha maswali na majibu, Sitta naye alijikuta kwenye masuala ya uchaguzi wakati alipomuombaparoko wa Parokia ya Urambo Mashariki kumuombea dua ili aweze kurudi bungeni mwaka 2011.
Spika, ambaye amekuwa akidai kuwa mafisadi wanamuandama kwenye jimbo lake na wakati fulani kuomba aongezewe ulinzi, alitoa kauli hiyo wakati akitambulisha wageni waliofika bungeni jana baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu.
Alikuwa akitambulisha kikundi cha wanakwaya 36 kutoka Urambo ambacho kilitembelea Bunge jana kikiwa safarini kuelekea jijini Dar es Salaam kurekodi albamu yao.
“Jamani mwaka huu ni mgumu kweli, kwa hiyo nyinyi watu wa dini mtuombee sana kwa Mungu kwa sababu hali ni ngumu kwetu,†alisema Spika Sitta.
“Kwa hiyo mkirudi jamani, mtuombee na mumwambie Baba Paroko Mongela atuombee ili aliyebora apite Urambo Mashariki.
“Sio lazima mimi lakini atuombee ili aliyebora apite na kuwa mbunge katika jimbo la Urambo Mashariki mkoani Tabora.â€
Wakati akiwatambulisha wanakwaya hao wa Kikundi cha Mtakatifu Cecilia kutoka Urambo, Sitta alisema kikundi hicho kinaongozwa na mwalimu kutoka Kenya ambaye anafundisha shule ya kimataifa ya mtakatifu huyo.
Baadaye akaipigia debe shule hiyo akisema: “Jamani sio muwapeleke (watoto) kwenye shule za mjini, hata shule za vijijini kama shule yetu ya kimataifa ya Urambo Mashariki.
“Halafu, Waziri wa Maji, shule yetu ile ya kimataifa ya Urambo haina maji, kwa hiyo nakuomba ufanye utaratibu wa kutupatia maji.â€

Rais Barack Obama ambaye alikuwa mwenyeji wa mkutano huo amewataka viongozi duniani kuchukua hatua ya pamoja kuzuia makundi ya kigaidi kupata silaha za nyuklia, hatua ambayo amesema itaifanya Marekani na dunia kwa ujumla kuwa na usalama. Akitoa hotuba ya mwisho ya kufunga mkutano huo kuhusiana na usalama wa nyuklia, amesema mkutano huo ni thibitisho tosha la nini kinachowezekana, iwapo mataifa yataungana pamoja kwa ari ya ushirikiano katika wajibu wa pamoja kukabiliana na changamoto. Katika taarifa ya pamoja ya viongozi waliohudhuria mkutano huo, waliunga mkono wito uliotolewa na Rais Obama wa kudhibiti vyema malighafi za nyuklia zilizo na uwezekano wa kuathiriwa katika muda wa miaka minne ijayo. Katika harakati za kupambana na biashara haramu ya silaha za nyuklia viongozi hao wamekubaliana pia kushirikiana kupeana taarifa na upelelezi, mahakama na utaalamu mwingine wa kisheria katika kushughulikia tatizo hilo. Viongozi hao wamesema wametambua mahitaji ya kushirikiana miongoni mwa mataifa kuweza kuzuia kikamilifu matukio ya biashara haramu ya nyuklia. Akiwa mwenyeji wa mkutano mkubwa kuwahi kufanyika nchini Marekani kwa zaidi ya miongo sita iliyopita, Rais Obama pia ameishinikiza China na wanachama wengine wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambao wana mashaka kuunga mkono vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran kuhusiana na mpango wake wa nyuklia wenye utata. Akizungumza katika mkutano huo kuhusiana na suala hilo la Iran, Rais Hu Jintao wa China amesema nchi yake kwa hakika inapinga silaha za nyuklia, lakini inaunga mkono matumizi ya nyuklia kwa raia.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, akisalimia na Rais wa China Hu Jintao .Kwa upande wake Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, ambaye ameunga mkono azimio lililofikiwa katika mkutano huo, ameelezea kufurahishwa kwake na hatua hiyo iliyofikiwa na China ya kuonesha uwezekano wa kuchukuliwa hatua dhidi ya Iran. Mbali na kuizungumzia Iran Rais Obama pia alielezea hofu iliyopo kuhusiana na maghala ya silaha za nyuklia nchini Pakistan, nchi ambayo ni ngome kubwa ya mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda na makundi mengine ya wapiganaji. Hata hivyo amesema nchi hiyo na nyingine ziko katika hatua ya kukabiliana na hali hiyo ikiwemo kutangaza hatua mpya ya kuimarisha usalama katika bandari kuzuia biashara haramu ya nyuklia. Naye Rais Dmitry Medvedev wa Urusi ameuelezea mkutano huo kama wa mafanikio wakati nchi yake ikiwa imetangaza mipango ya kufunga mtambo wake wa mwisho wa madini ya Plutonium ambayo ni ya sumu kali yanayotumika kutengenezea silaha za nyuklia.
Rais wa Marekani Barack Obama na Rais wa Urusi Dmitry Medvedev wakati wa mkutano wa usalama wa nyuklia, mjini Washington. Afisa wa Urusi ambaye hakutaka jina lake litajwe, alilithibitishia shirika la habari la AFP kwamba Rais Medvedev alitangaza mipango hiyo katika mkutano wa Washington. Mkutano mwingine wa usalama wa nyuklia unatarajiwa kufanyika Korea ya Kusini miaka miwili ijayo. Mwandishi: Halima Nyanza(afp,Reuters) Mhariri: Josephat Charo

Kwa mara ya kwanza katika historia ya siasa za Uingereza, viongozi wa vyama vikuu vitatu vya kisiasa nchini humo wameshiriki mdahalo wa uchaguzi wa nafasi ya waziri mkuu.
Mdahalo huo ulionyeshwa moja kwa moja kupitia televisheni.
Waziri mkuu Gordon Brown, na wapinzani wake, David Cameron wa chama cha Conservative na Nick Clegg wa Liberal Democrats, walijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na watu walioalikwa kwenye mdahalo huo.
Maswali hayo yalihusu mada mbalimbali ikiwa ni pamoja na uhamiaji na namna ya kutatua suala la nakisi ya bajeti ya Uingereza.
Midahalo mingine miwili ya televisheni ikilenga masuala ya nje na uchumi wa Uingereza, imeandaliwa kufanyika kabla ya siku ya uchaguzi , tarehe sita Mei mwaka huu.
Maoni ya haraka baada ya mdahalo huo yamempa ushindi bwana Clegg ambaye chama chake kinaweza kuleta uwiano katika uongozi wa nchi hiyo baada ya uchaguzi.

MWENYEKITI wa Chama cha Democrat (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu Mkoa wa Dar es Salaam kwa tuhuma za kuandaa na kusambaza waraka unaodaiwa kumkashifu Rais Jakaya Kikwete.
Tanzania Daima ilipata taarifa kuwa maofisa wa polisi kutoka Makao Makuu pamoja na Kanda Maalum ya Dar es Salaam waliokuwa wakiongozwa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda ya Dar es Salaam (ZDCO), Charles Mkumbo, walizingira nyumba ya Mtikila iliyopo Mikocheni B.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, askari hao walianza kufanya upekuzi katika nyumba hiyo jana, majira ya saa moja na nusu asubuhi baada ya kusikia taarifa za waraka huo uliokuwa umehifadhiwa kwenye kompyuta ya Mtikila.
Wakati maofisa hao wa polisi wamezingira nyumba hiyo, Mtikila na mkewe, Georgia Mtikila walilipigia simu gazeti hili, kuliarifu tukio hilo ambalo lilifanyika bila purukushani zozote.
Mtikila alisema katika upekuzi huo, askari hao waliichukua kompyuta moja inayodaiwa kuhifadhi waraka huo, wakaondoka naye hadi Kituo Kikuu cha Polisi kwa mahojiano zaidi.
Alisema timu ya maofisa wa polisi ilianza kumhoji kwa njia ya mdomo kuanzia saa nne asubuhi hadi saa nane mchana yalipomalizika ambapo aliomba aruhusiwe kutoka nje ili amuagize mkewe akamfuate wakili wake.
Kiongozi huyo alisema alifanya hivyo ili wakili wake awepo wakati polisi wanaanza kuchukua maelezo yake kwa maandishi.
Mtikila alisema alielezwa kuwa jeshi hilo lilifikia hatua ya kumkamata kwa sababu anakabiliwa na tuhuma za uchochezi kutokana na hatua yake ya kuandika waraka wa kutetea Ukristo, wenye kurasa 24.
Alisema katika waraka huo, amewataka Wakristo waungane ili waweze kumchagua rais Mkristo kwenye uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba.
Mtikila alisema kama Wakristo wakifanya hivyo, watakuwa wameunusuru Ukristo ambao hivi sasa upo shakani kutokana na kukandamizwa na utawala uliopo, ambao kwa mujibu wake unapendelea Uislamu.
“Polisi walinikamata asubuhi nyumbani kwangu wakachukua kompyuta yangu…na katika mahojiano yetu sijaukana ule waraka nimekubali ule waraka ni wangu kwani ili kuukana ule waraka nitakuwa namkana Yesu Kristo na mwokozi wangu.
“Serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Kikwete imeutesa Ukristo kuliko kipindi chochote kile tangu Ukristo uje nchini… ndiyo maana ni kosa la jinai katika awamu ya nne kuutetea Ukristo, lakini ni halali kwa waumini wa dini ya Kiislamu kufanya mikakati yote kuuangamiza Ukristo,” alisema Mtikila na kuongeza kuwa waraka huo uko mbioni kuchapwa ili kiwe kitabu kamili.
Tanzania Daima liliwasiliana na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, ambaye alithibitisha kukamatwa kwa Mchungaji Mtikila.
Kamanda Kova alisema wanamshikilia kiongozi huyo kwa tuhuma za kuandaa waraka huo na kuusambaza kwa baadhi ya wachungaji wa dini, ukiwa na ujumbe unaoweza kuhatarisha amani nchini.
Alisema polisi walifikia hatua ya kumkamata baada ya kupata taarifa kutoka Idara ya Usalama wa Taifa, kwamba Mtikila ameandaa waraka huo na ameshausambaza kwa baadhi ya wachungaji.
“Ni kweli tunamshikilia Mtikila na tumefikia hatua ya kumkamata baada ya jeshi letu kupata taarifa hizo kutoka Idara ya Usalama wa Taifa, na tumemkamatia nyumbani kwake na kutokana na ukubwa wa tukio hilo, siwezi kulizungumzia, kwani jambo hilo liko chini ya Makao Makuu ya Polisi nchini,” alisema.
Hata hivyo, habari ambazo tumezipata wakati tunakwenda mitamboni, Mtikila ameachiwa kwa dhamana ya polisi na ametakiwa kuripoti leo saa nane mchana.
Hii si mara ya kwanza Mtikila kukamatwa kwa tuhuma za uchochezi, kwani mwaka juzi alikamatwa na kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kosa la kusambaza waraka wa kumkashifu Rais Kikwete kwa kumuita gaidi anayetaka kuleta Mahakama ya Kadhi nchini.
Mtikila alibainisha kuwa, katiba ya nchi inatamka bayana kuwa Tanzania si nchi ya kidini. Kesi hiyo inaanza kusilizwa Aprili 22, mwaka huu.
Vile vile, Mtikila alishawahi kufikishwa katika mahakama hiyo akikabiliwa na kesi ya kutoa maneno ya uchochezi wakati akihutubia katika mkutano wake katika Viwanja vya Jangwani kwa kumkashifu Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere.
Mchungaji huyo alishawahi kushinda kesi ya kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa alipomwita rais wa Msumbiji anayeuza nchi kwa Wazungu.

POLISI jijini Dar es Salaam wamemkamata Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila wakimtuhumu kusambaza waraka wenye nia ya uchochezi.
Kwa mujibu wa mke wa Mtikila, Georgia, mwanasiasa huyo amekamatwa leo saa mbili asubuhi nyumbami kwake Mikocheni, Dar es Salaam.
Georgia amesema, takrinani polisi 12 walikwenda nyumbani kwa Mtikila wakati mchungaji huyo akiwa chumbani kwake.
Amewakariri polisi hao wakidai kuwa walikwenda kumkamata Mtikila, na kwamba pia walichukua kompyuta ya mwanasiasa huyo wakidai kuwa wanakwenda kuichunguza.
“Baada ya kuingia wakidai kumhitaji Mchungaji, alitoka na kuwaambia wamsubiri avae nguo ndipo aweze kuongozana nao kwa kuwa muda ule ndio kwanza alikuwa anaamka…aliwaambia kwa nini hamkunipigia simu ili nije peke yangu hadi mfikie hatua ya kuja kunichukua nyumbani kwangu,” alikaririwa Mama Georgia maneno aliyosema mumewe.
Inadaiwa kuwa, kati ya Julai na Septemba mwaka jana Mtikila aliandika na waraka wa uchochezi wakati akiwa Mwanza alipokwenda kuzungumza na viongozi wa kikristo.
Waraka huo ambao umesainiwa na Mchungaji Mtikila una maandishi ‘Kikwete kuangamiza kabisa Ukristo, wakristo wasipoungana upesi kuweka Mkristo Ikulu.
Georgia amesema, anahisi kwamba, Mtikila amekamatwa kwa sababu za kisiasa zaidi hasa ikizingatiwa kuwa amekuwa akishinikiza kuwepo kwa mgombea binafsi katika uchaguzi mkuu ujao.
“Hiyo ni kumtia kashkash tu ya kisiasa ili asijipange kama wagombea wengine, kwani waraka huo ulikuwa na nia ya kutetea imani kwa wafuasi wa dini ya kikristo haswa kusimamia ni kiongozi gani watakayemchagua,” amesema Georgia.

WAZIRI wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk John Magufuli, amekubali kurudisha katika Kamati ya Bunge, Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya miswada miwili kuhusu mifugo.
Hatua hiyo imekuja baada ya wabunge kadhaa, kupinga miswada hiyo kwa madai kuwa ilikuwa inalenga, kuwanyanyasa wafugaji.
Miswada hiyo ni ule wa utambuzi, usajili na ufuatiliaji wa mifugo ya mwaka 2010 na wa sheria ya malisho na vyakula vya mifugo wa mwaka 2010, iliyowasilishwa bungeni jana, lakini baadhi ya wabunge waligoma kuiunga mkono.
"Miswada hii ingepitishwa ingekuwa kitanzi kwa serikali maana isingefanya operesheni ya ajabu. Sheria hiyo ingeibana serikali," alisema Magufuli
Msimamo wa wabunge dhidi ya miswada hiyo iliyokuwa imewasilishwa bungeni na waziri Magufuli, ulianzishwa na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, alipomuomba Naibu Spika wa Bunge, Anna Makinda, atoe mwongozi wa kama anaweza (Ole Sendeka) kuomba miswada hiyo urudishwe na isijadiliwe na Bunge, hadi hapo utakapofanyiwa mabadiliko.
Mbunge huyo alisema kifungu cha 61 na 69 kinatoa mwongozo kuwa mbunge anaweza kuomba hoja inayojadiliwa irejeshe kuandaliwa upya na kujadiliwa tena na Bunge.
Kutokana na hoja hiyo Naibu Spika Anna Makinda aliamua kumuokoa waziri Magufuli, kwa kumtuliza mbunge huyo kuwa kifungu cha 61 kiko wazi na kimtaka mbunge aeleze sababu za ombi.
Alisema hata hivyo kwa kuzingatia umuhimu wa muswada huo, anatumia kifungu cha 69 kuruhusu majadiliano yaendelee ili serikali ipate mawazo zaidi kuhusu na miswada hiyo.
"Kwa mamlaka niliyonayo nami natumia kifungu cha 61 kifungu kidogo cha 2 kuruhusu mjadala huu uendelee ili serikali ipate mawazo ya wabunge wengine. Mjadala unaendeleo†alisema Makinda
Hata hivyo uamuzi huo ulichochea moto kwa mbunge aliyefuata kukosoa miswada hiyo.
Mbungwe huyo, alikuwa ni George Simbachawene (Kibakwe) ambaye alipinga vikali muswada wa utaifishaji wa mifugo ya wafugaji kwa kisingizio ya kuwa mingi.
"Sheria hii ina lengo la kuwafuta wafugaji, mnaweka sheria ya kusajili mifugo yao wakati tumeshindwa kusajili magari, nenda Dar magari yamerundikana watu wameshindwa kusajili, kabla ya kusajili mifungo hebu tuanze kwanza na magari haya tuondokane na msongamano barabarani," alisema.
Kwa upande wake, Mbunge wa Longido (CCM) Michael Lekure, alipinga kuunga mkono muswada huo kwa maelezo kuwa hauzingatii utawala bora
"Nilitegemea muswada huu utazingatia utawala bora, na ungewasaidia wafugaji lakini badala yake, umeonyesha kuwa ni wa kuwanyanyasa," alisema.
"Kwa sababu moja au nyingine siuungi mkono muswada huu," alisisitiza mbunge huyo.
Lazier alisema kwa yeye kuunga mkono miswada hiyo ni sawa na kuwasaliti wafugaji ambao walimpigia kura pamoja na Chama Cha Mapinduzi, ili awawakilishe katika Bunge.
Aliungana na Ole Sendeka kutaka muswada huo urudishwe na kuandaliwa upya kabla ya kuwasilisha tena bunge kwa majadiliano.
Mbunge wa Kiteto (CCM) Benedict Ole Nangolo, alisema muswada ni nakala ya utafiti wa mwanafunzi wa shahada ya falsafa ya Udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Texas nchini Marekani.

WAKATI fulani Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema yuko tayari kusulubiwa kuliko kuzungumzia masuala ya kampuni za Tangold, Meremeta na Mwananchi, lakini msimamo huo haukumzia mbunge wa Karatu, Dk Willibrod Slaa kuibua tena swali kuhusu kampuni hizo, akitaka hatima ya malalamiko ya wabunge.
Mara kadhaa, Dk Slaa amekuwa akimbana Pinda kuhusu kampuni hizo zinazolalamikiwa kuwa zilichota mabilioni ya fedha za walipa kodi kwa njia za kifisadi, lakini serikali imekuwa ikieleza kuwa kampuni hizo zinahusu masuala ya usalamwa taifa na hivyo hayawezi kuzungumziwa hadharani.
Na alipobanwa sana, Pinda alijibu yuko tayari kusulubiwa.
Jana Dk Slaa aliibua tena hoja hiyo katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa waziri mkuu na kumtaka kiongozi huyo wa shughuli za serikali bungeni aeleze hatima ya sakata la kampuni hizo.
Dk Slaa, ambaye pia ni katibu mkuu wa Chadema, alisema kuwa kwa karibu mwaka mmoja sasa tangu ufisadi huo ulipoibuliwa, kumekuwa na kauli mbalimbali kuhusu kampuni hizo ambazo haziridhishi na ambazo wakati fulani mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe aliwahi kuziita za ovyo.
Kutokana na hali hiyo, Dk Slaa alimtaka waziri mkuu atoe tamko la serikali pamoja na kufafanua hatua ilizofikia katika kuwashughulikia wahusika wa ufisadi huo.
Swali hilo lilimfanya waziri mkuu, maarufu kama mtoto wa mkulima, kupatwa na kigugumizi kujibu akieleza kuwa hawezi kuwa na majibu ya moja kwa moja kuhusu kampuni hizo.
“Ndugu yangu Dk Slaa anajua siwezi kuwa na majibu ya moja kwa moja, ila ninachoweza tu kusema ni kuwa maeneo ambayo serikali imeshayafanyia kazi na jitihada zake zimeanza kuonekana," alisema Pinda.
"Pia yapo yale ambayo bado yanaendelea kufanyiwa kazi.â€
Hata hivyo pamoja na majibu hayo, Dk Slaa aliuliza swali la nyongeza akitaka Pinda atoe tamko kuhusu ufisadi huo kwa kuwa ndiye kiongozi wa shughuli za serikali bungeni.
“Waziri mkuu ninakuheshimu sana, kwa vile katiba inasema wewe ndiye msimamizi wa serikali hapa bungeni, usipojibu wewe maswali haya magumu nani atajibu," aliuliza Dk Slaa.
"Basi ninakuomba utoe tamko kuhusu jambo hili bungeni na maeneo yaliyoshughulikiwa.â€
Lakini, hata hivyo waziri mkuu hakuweza kufafanua zaidi kuhusiana na eneo ambalo limeshughulikiwa na serikali na lile ambalo bado huku akisisitiza kuwa kauli alishatoa na kwamba serikali imeshachukua hatua.
Pinda alisema hatua hizo ni pamoja na za kimahakama katika masuala yaliyohusu sheria na kumuomba Dk Slaa aeleze iwapo kuna mahali ambapo anadhani bado serikali haijashughulikia.
“Ndugu yangu, kama unataka kauli nimeshaitoa. Nimeeleza kuwa yapo mambo ambayo tayari yameshughulikiwa na kufikishwa mahakamani, kama bado kuna mengine, itoshe kusema kuwa serikali itaendelea kuyafanyia kazi na kuyashughulikia,†alieleza Waziri Pinda.
Dk Slaa amekuwa akiibua sakata la makampuni hayo kila mara na mwaka jana alikumbwa na vikwazo kadhaa wakati alipotaka kusoma maoni ya kambi ya upinzani kuhusu hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
Wakati huo, Spika Samuel Sitta alitangulia kumuonya kuhusu mambo kadhaa, ikiwemo matumizi ya maneno dhidi ya rais wa zamani na suala hilo la kampuni hizo, hali iliyomfanya mbunge huyo wa Karatu kuruka sehemu nyingi za hotuba yake.
Hata hivyo, alihoji suala la kampuni hizo tatu na Spika Sitta alilimaliza kwa kumwambia kuwa walishakubaliana kwenye vikao vya kamati za Bunge kuwa masuala yanayohusu jeshi yasizungumziwe hadharani.